Skip to main content




AINA ZA SENTENSI
Kuna aina kuu nne za sentensi
Sentensi changamano
Sentensi sahili/ huru.
3. Sentensi shurutia
Sentensi Ambatano
1.SENTENSI SAHILI/HURU
Hii ni aina ya sentensi ambayo hutawaliwa na kishazi huru. Kishazi hicho kinaweza kuwa kifungu tenzi kimoja ambacho kinaweza kuwa na kitenzi kikuu au kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu au kitenzi kishirikishi na shamirisho
Mfano: Juma ni mzembe
Juma alikuwa mzembe sana
Mwalimu alikuwa nafundihsa darasani


MIUNDO YA SENTENSI HURU /SAHILI
Muundo wa kitenzi kikuu peke yake (tawaliwa)
Mfano: Wanacheza
Alinipiga
Wanasoma
i.Muundo wa kitenzi kikuu peke yake (tawaliwa)
Mfano: Wanacheza
Alinipiga
Wanasoma
ii.Muundo wa kitenzi na kitenzi kikuu
Mfano: Alikuwa anasoma
Walikuwa wanataka kufundishwa
ii Muundo wa kirai na kirai kitenzi
Mfano; Mwalimu anafundisha
Wanafunzi wanamsikiliza
iii. Muundo wa virai vitenzi vilivyokitwa katika kitenzi kuwa
Mfano: John alikuwa kijana mzuri
Mwalimu atakuwa darasani
Aisha angekuwa wa kwanza


V.Muundo ambapo virai nomino na virai kitenzi vinaambatana na vijalizo
Mfano: Baba yangu alinunua machungwa mawili usiku


SIFA ZA SENTENSI SAHILI/HURU
1. .Inakiima ambacho kinaweza kutajwa wazi au kisitajwe kama kinaeleweka.
2. Inakiungo ambacho kinaunda kitenzi kikuu kimoja au kitenzi kiuu c akitenzi kisaidizi au kitenzi kuku na shamrisha na chagizo
3. Haifungamani na sentensi nyingine na inajitosheleza kimuundo na kimaana
UCHANGANUZI WA SENTENSI SAHILI
Kuchanganua sentensi ni kitendo au mbinu ya kuitenga au kuigawa sentensi katika sehemu mbalimbali ambazo hujenga au kuiunda sentensi hiyo. Kuna mikabala mikuu miwili ya uchanganuzi wa sentensi,
1. Kwa kutumia mkabala wa kimapokeo ambapo sentensi hugawanywa katika kiima na kiarifu na baadaye hufuatiwa na vipashio vinavyojenga kiima na kiarifu



iii. Mkabala wa kimuundo/ kisasa ambapo sentensi hugawanywa katika sehemu kuu mbili yaani kirai nomino na kirai kitenzi kisha hufuatwa na vipashio vijengavyo kirai nomino na kirai kitenzi
Mfano; Wanafunzi wale walikua wanasoma darasani




N:B
Katika uchanganuzi wa sentensi ni muhimu kutofundishwa mikabala yote miwili (haipaswi)
Lakini kuna baadhi ya wataalamu wanachanganya mikabala yote Miwili katika uchanganuzi wao wa sentensi. Mfano; F.Nkwera (1978) TUMI (1988) J.S.Mdee (1996) Mohamed Taasisi ya dimu (1966)


UCHANGANUZI WAKE
i. Kutaja aina ya sentensi
ii Kutaja sehemu za sentensi yaani kiima/kikundi nomino, kiarifu/kikundi kitenzi
iii Kutaja vipashio vinavyojenga kiima na kiarifu
iv.Kutaja aina za maneno yote yaliyomo katika sentensi
v.Kuandika upya sentensi hiyo.
AINA ZA UCHANGANUZI WA SENTENSI
Uchanganuzi wa sentensi hufuata
i.Mishale/ mistari
ii.Matawi/msonge/ngoe
iii.Maelezo/maneno
iv.Parandesi/mabano
v jedwali/visanduku
1. UCHANGANUZI WASENTENSI SAHILI
NJIA YA MANENO
A.MKABALA NA KIMPOKEO
i. Mtoto Yule alikuwa anataka kucheza mpira wake uwanjani
Hii ni sentensi sahili
Kiima ni mtoto Yule
Kiima kinanomino na kivumishi
Nomino ni mtoto
Kivumishi ni Yule
Kiarifu ni alikuwa anataka kucheza mpira wake uwanjani
Kiarifu kina vitenzi visaidizi viwili kitenzi kikuu, shamrisho, chagizo
Kitenzi kisaidizi cha kwanza ni alikuwa
Kitenzi kisaidizi cha pili ni anataka
Kitenzi kikuu ni kuchezea
Shamirisho ni mpira wake
Nomino ni mpira
Kivumishi ni wake
Chagizo ni uwanjani
Kielezi ni uwanjani

B.MKABALA WA KISIASA
Mtoto yule alikuwa anataka kuchezea mpira wake uwanjani
Hii ni sentensi sahili
Kirai nomino ni “mtoto Yule”
Kirai nomino kina nomino na kivumishi
Nomino ni mtoto
Kivumishi ni Yule
Kirai kitenzi ni alikuwa anataka kucheza mpira wake uwanjani
Kirai kitenzi kina vitenzi visaidizi viwili kitenzi kikuu kirai,nomino na kirai kielezi
Kitenzi kisaidizi cha kwanza ni alikuwa
Kitenzi kisaidizi cha pili ni anataka
Kitenzi kikuu ni kucheza
Kirai nomino kina nomino na kivumishi
Nomino ni mpira
Kivumishi ni wake
Kirai kielezi kina kielezi
Kielezi ni uwanjani


ii. NJIA YA MISHALE
A. MKABALA WA KIMAPOKEO
Mtoto Yule alikuwa anataka kucheza mpira wake uwanjani


B. MKABALA WA KISASA




III. NJIA YA MATAWI




IV. NJIA YA JEDWALI
A. MKABALA WA KIMAPOKEO



S.SAHILI

K
A


P
SH

N
T
N
V

JUMA
NI
MTOTO
MWEMA



B. MKABALA WA KISASA





S.SAHILI

KN
KT


P
KN

N
T
N
V

JUMA
NI
MTOTO
MWEMA





2.SENTENSI CHANGAMANO
Ni sentensi inayotawaliwa na kishazi huru kimoja au zaidi, na kishazi tegemezi kimoja au zaidi. Kishazi huru/tegemezi hicho kinaweza kutokea upande wa kiima au kiarifu
Mfano: Wanafunzi waliotoroka jana wameadhibiwa leo asubuhi
B
Mwalimu amewaadhibu wanafunzi waliotoroka jana
B
NB: Sifa kubwa ya sentensi changamano ni kuwa na kishazi tegemezi ambacho hutegemea kishazi huru kilichomo ndani ya sentensi hiyo.
MIUNDO YA SENTENSI CHANGAMANO
Vishazi tegemezi vilivyomo ndani ya sentensi changamano ndiyo hutupatia miundo mbalimbali ya sentensi.


Hii ni miundo ambayo kirai nomino hubeba kishazi tegemezi kirejeshi ambacho hurejesha tendo kwa mtenda au mtendwa
Mfano: Mbuzi aliyenunuliwa juzi ameibwa leo asubuhi
BV


Miundo yenye vishazi tegemezi vielezi
Hii ni miundo ambayo vishazi tegemezi hurejelewa/hueleza hali ya vitenzi vilivyomo kutoka vishazi huru
Mfano: Mimi sikuvutiwa alivyosema
BE
Juma aliponiona alikimbia
BE


UCHANGANUZI WA SENTENSI CHANGAMANO
Uchanganuzi wa sentensi changamano huwa na hatua zifuatazo
i.Kutaja aina ya sentensi
ii.Kutaja kiima/kirai nomino na kiarifu/kirai kitenzi
iii.Kutaja vishazi vilivyomo katika sentensi nakishakueleza kazi ya kila kishazi


Kwa mfano: Kutaja kama kishazi tegemezi kinavumisha jina au kikundi jina kilichopo katika kiini
Mfano: Mbuzi aliyenunuliwa juzi ameibwa leo asubuhi
BV
Mwalimu aliwaadhibu wanafunzi waliotoroka
Bv
b. Kutaja kama kishazi tegemezi kinavumisha nomino au kikundi nomino kilichopo katika shamirisho.
c. Kutaja kama kishazi tegemezi kinatoa maelezo zaidi kuhusu kitenzi kikuu kilichopo katika kishazi huru
Mfano: Juma aliponiona alikimbia
BE
Juma alikimbia aliponiona
BE
Iv Kutaja aina zote za maneno katika sentensi hiyo
V.Kurudia kuandika sentensi hiyo
I. NJIA YA MATAWI.
A: MKABALA WA KIMAPOKEO
Mtoto aliyekuletea maji ya kunywa ni mwanangu



Mtoto aliyekuletea maji ya kunywa ni mwanangu





SENTENSI SHURUTIA
Ni sentensi ambayo huwa na vishazi tegemezi viwili ambavyo utegemezi wake hutokana na mofimu “nge”- ngali –ngeli na –ki-. Mofimu hizi hufanya vishazi hivyo vitegemeane yaani kufanyika kwa tendo moja kunategemea tendo jingine au kutokuendeka kwa jambo fulani hutegemea kutokutendeka kwa jambo Fulani,
Mfano: Juma angejibu maswali yote angefaulu mtihani
- Ukisoma kwa bidii utafaulu mtihani
N:B Mofimu hizi zinapotumika katika sentensi shurutia huwa hazitakiwi kuchanganywa
SWALI: Huku ukitumia mifano onesha tofauti iliyopo kati ya sentensi na tungo
NGELI ZA MAJINA (NOMINO)
Neno ngeli ni neno la Kiswahili lililotolewa kutoka lugha ya kihaya likiwa na maana ya vitu vinavyofanana au vinavyoshabihiana.
Kwa hiyo ngeli za nomino na makundi ya majina yanayofanana au yanayowiana kwa kutuma kigezo Fulani. Nomino za lugha ya Kiswahili zinaweza kuwekwa katika makundi yanayofananana kwa kutumia vigezo vikuu viwili.
i. ) Kwa kutumia kigezo cha mofolojia ya maneno hayo ambacho huyapanga majina kwa kuangalia maumbo ya umoja na wingi wa majina hayo.
ii.) Ni kigezo cha kisintaksia ambacho huyagawa majina katika makundi yanayowiana kwa kuzingatia uhusiano uliopo baina ya majina na vitenzi.Majina yote yanayohusiana kwa namna moja au kwa namna inayofanaa yanapoishia na vitenzi hufanya kundi moja la ngeli.
KIGEZO CHA KIMOFOLOJIA/MAUMBO YA UMOJA NA WINGI
Hiki ni kigezo kilichotumika na wanasarufi wa mwanzo ambao waliainisha majina kulingana na maumbo ya umoja na wingi au viambishi awali vya majina hayo. Majina hayo yanayofanana katika viambishi awali yaliwekwa katika kundi moja na kufanya kundi moja la ngeli. Kama sarufi hao wapo walioyagawa majina katika makundi kumi na nane(18) na uongozi ulioyagawa majina hayo katika makundi tisa (9) lakini kwa kutumia kigezo hicho hicho cha kimafolojia kwa kutumia kigezo hiki tutayafafanua makundi ngeli kumi na nane (18) za majina ya Kiswahili.



NGELI
SIFA ZA MAJINA
MFANO

1.Mu
-Majina ya viumbe hai isipokuwa mimea
m-tu wa –tu

2.Wa
-Vitenzi jina vyote vinavyotaja watu vina
m-toto wa- toto



-Vitenzi jina vyote vinavyotaja watu
Vinavyoanza na “m” katika moja na “wa” katika wingi
m-fungaji wa fugaji

3.M-
-Majina ya baadhi ya mimea
m-ti mi –ti

4Mi-
-Majina ya vitu vyote vinavyoanza na “M” katika umoja na “mi”katika wingi
m-papai mi – papai
m-pir mi-pira
M-sumeno mi-sumeno



-Majina ya matendo/vitenzi jina vinayoanza na “m” katika umoja na “mi” katika umoja na “mi” katika wingi
m-kasi mi-kasi
m-chezo mi- chezo
m-tupo mi-tupo

5.Ki





6 vi-
-Majina yote yanayoanza na “ki-“ katika umoja na “vi-“ katika wingi
Ki-nu vi-nu
Ki-kapu vi-kapu
Ki- umbe vi- umbe



-Majina ya vitu vinayoanza na “ch” katika umoja na “vy” katika wingi
ki-goda vi-goda
ch-akula vy-akula
ch-uma vy-uma



-Majina ya viumbe yanayoambikwa kiambishi”ki” mwanzoni cha kuvumisha
Ki-zee vi-zee
Ki-vulana vi-vulana
Ki-toto vi-toto

7.Ji-
-yanaingia majina yanayoanza na



8.Ma
Ji-katika umoja na wingi
Ji-cho ma –we



-Majina ya baadhi ya sehemu sa mwili wa binadamu wanyama au sehemu za mtu
Ji – cho ma-cho
Goti ma-goti
Ji-no meno



-Majina ya mkopo yenye kuanzana “ma” katika wingi
Sikio ma-sikio
Maziwa maziwa



-Majina yenye kueleza dhana ya wingi japokuwa hayahesabiki
Shati ma-shati
Bwana ma – bwana
Ua ma - ua



-Majina yote yanayoanzia na N-na kufuatwa na konsonati ch, d, g, j, z, y katika umoja na wingi
Njaa,nguo, nchi, ndoa nzi
Nje, nyumba

9 N
-Majina yanayoanza na M- na Mb
Mbuga, mboga, mvua mvinyo, mvi, mbao, taa

10
-Majina ya mkopo





N:B: Maumbo ya umoja na wingi katika majina haya haya badiliki
Kalamu

11U
12N
-Majina yote yanayoanza na
U- katika umoja na N-au
Mb- katika wingi
U-so N-nyuso
U-zi N-yuzi
U – bao Mb – ao
u-limi ndimi

13 U
-Majina yote yanayoanza na
U-asi ma – asi

14Ma
U – katika umoja -ma-
Katika wingi
U-gonjwa ma – gonjwa
U-gonjwa ma-gonjwa

15 ku
Majina yanayotokana na vitenzi vinavyoonea ku- mwanzoni
Ku – imba
Ku –cheza
Ku-la

16. Pa
Huonesha mahali pa mbali
Kidogo palipo wazi
pahala

17. Mu
Kuonesha mahali pa mbali lakini ndani
Mule

18.ku
Mahali pa mbali zaidi
kule



FAIDA ZA UAINISHAJI NGELI KIMOFOLOJIA
1. Hutumika kuonesha uhusiano wa lugha zenye asili moja
Mfano: Lugha ya Kiswahili na lugha mbalimbali za kibantu. Majina mengi ya lugha ya Kiswahili yana maumbo dhahiri ya umoja na wingi pia majina mbalimbali ya lugha za kibantu yana sifa hiyo.


2. Ni rahisi kugawanya majina hasa yale yenye maumbo ya umoja na wingi katika makundi mbali mbali kwa kutumia kigezo hiki.
3. Kutumika kuonesha maumbo ya umoja na wingi katika nomino


MATATIZO YA UAINISHAJI KIMOFOLOJIA
1. - Ni vigumu kuyapanga majina yasiyokuwa na maumbo ya umoja na wingi katika makundi yake kwa kutumia vigezo hiki.
2. - Hakitilii maanani miundo ya sentensi kwa mfano nomino kama kipofu, kiongozi, kijana, zilipaswa kuwa katika ngeli ya ki-vi lakini zimepelekewa katika ngeli ya kwanza kwa kuwa zinaoana kimuundo na nomino nyingine za kundi hilo. Nomino hizo kimefolojia zinatofautiana na nomino nyingine za ngeli ya kwanza na ya pili.
3. - Hakikidhi mahitaji ya sulubu na sentensi .
Mfano: Kitabu changu kimepotea
Vitabu vingi vimepotea
Kisu changu kimepotea
Visu vyangu vimepotea
Kijana wangu amepotea
Vijana wangu wamepotea
Baadhi ya nomino hazikidhi sababu za sentensi
4. Kuna viambishi vya ngeli vinavyofanana na kujirudia rudia kwa baadhi ya makundi ya majina. Mfano kiambishi mu – kinajitokeza katika ngeli ya makundi ya majina. Mfano kiambishi mu – kinajitokeza katika ngeli 3; ngeli kiwakilishi ma-cha ngeli ya 8; kinajitokeza katika ngeli ya 1
Kiambishi N. Kinajitokeza katika ngeli ya kumi na mbili pia kinatumika katika ngeli ya tisa na ya kumi.
KIGEZO CH A KISINTAKSIA
Hiki ni kigezo ambacho huyagawa majina katika makundi mbalimbali kutokana na kigezo cha upatanisho wa kisarufi uliopo kati ya maji na viambishi awali vilivyopo katika vitenzi ambavyo huyapatanisha majina hayo na vitenzi.
Majina yote yanayotumia viambishi awali vipatanishi vinavyofanana huwekwa katika kundi moja na kufanya kundi moja la ngeli. Kwa kutumia kigezo hiki kuna jumla ya ngeli tisa za nomino





NGELI
Viambishi awali vipatanishi
Mfano

a -wa
a -wa
Kiongozi amepotea/viongozi wamepata



a-umoja,
Simba amepotea/simba wamepotea



wa-wingi



u-i
u-(umoja)
Mto umefunika



i-(wingi)
Mito imefunika





Mti umeanguka





Miti imeanguka

Li - ya
li-(umoja)
Yai limevunjika



Ya-(wingi)
Mayai yamevunjika





Gari limetengenezwa





Magari yamebaribika

Ki-vi
Ki – (umoja)
Kiti kimevunjika



Vi-(wingi)
Viti vimevunjika





Chakula kimemwagika





Vyakula vimemwagika

i-zi
i-(umoja)
Nchi imefilisika



Zi-(wingi)
Nchi zimefilisika

u-zi
u-(umoja)
Ukuta umebomoka



Zi(wingi)
Kuta zimebomoka





Ubao umechafuka





Mbao zimechafuka

u-ya
u-(wingi)
Ugonjwa umeenea



Ya-(wingi)
Magonjwa yameenea





Ubaya umeongezeka





Mabaya yameongezeka

ku
Ku-
Kucheza kunafurahisha





Kula kwake kunasikitisha





Kuimba kwao kunapendeza

Pa


Pale panapendeza

Mu


Mule mwanagiea

Ku


Kule kunapendeza



FAIDA ZA KIGEZO HIKI
1. - Hutumika kama kigezo cha ulinganifu wa lugha haswa Kiswahili na lugha za kibantu
2. - Hutumika kuyapanga majina katika makundi yanayofanana
3. -Huweza kuyaweka majina katika makundi kiurahisi zaidi hata yake yasiyokuwa na maumbo ya umoja na wengi ilimradi yahusiane kisarufi


MATATIZO YA KIGEZO HIKI
1. Katika ngeli ya kwanza kuna vipatanishi viwili vya umoja ambavyo ni yu na-a- kiambishi yu – ni cha Kiswahili cha kilahaja sio Kiswahili sanifu.
2. Huyaweka majina yenye maumbo na sifa tofauti katika kundi moja. Mfano nomino za kipekee kama vile Juma Amina Latifa na zile za kawaida kama vile chura, kaka ,mama , baba
3. Kuna baadhi ya majina ambayo viambishi vipatanishi vina utata hivyo inakuwa vigumu kuyainisha mfano: Jambazi amepigwa risasi /majambazi yamepigwa risasi
4. Kuna vipatanishi vinavyofanana katika ngeli.Mfano kiambishi -u- cha umoja katika ngeli ya pili kinajitokeza katika ngeli ya sita na ngeli ya saba. Kiambishi kipatanishi i – cha wingi cha ngeli ya pili kinajitokeza katika ngeli ya tano umoja na kiambishi patanishi “zi” wingi cha ngeli ya tano kinajitokeza katika ngeli ya sita wingi
MATUMIZI YA NGELI
1. Hutumika kuyapanga majina katika makundi yanayoshabihiana kwa kutumia kigezo maalumu mfano: kimofolojia na kisintaksia
2. Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika nomino na vivumishi. Mfano;
M-toto, m-zuri
Ki-tabu ki-zuri
3. Hutumika kuonesha upatanishi wa kisarufi uliopo kati nomino, vivumishi na vitenzi mfano: Mtoto mzuri amepata
-Kitu kizuri kimepotea
4. Hutumika kuonesha uhusiano baina ya lugha ya Kiswahili lugha mbalimbali za kibantu

Popular posts from this blog

FASIHI KWA UJUMLA NADHARIA YA FASIHI SANAA Sanaa ni uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifu umbo ambalo msanii hulitumia katika kufikishia ujumbe aliokusudia kwa jamii / hadhira. AINA ZA SANAA a) Sanaa za ghibu (muziki) Inategemea na matumizi ya ala za muziki (vifaa, sauti) uzuri wa umbo la sanaa ya muziki upo katika kusikia. Sanaa hii hailazimishi fanani (msanii) na hadhira kuwepo mahali pamoja kwa wakati mmoja. Mtunzi hufanya kazi kwa wakati wake na hadhira husikiliza kwa wakati wake. b) Sanaa za ufundi Sanaa hizi hutokana na kazi za mikono. (Mfano: uchoraji, ususi, ufinyanzi, uchongaji, uhunzi, utalizi/udalizi n.k.) Mfano; - uchoraji hutegemea sana kuwepo kwa kalamu, karatasi, kitambaa, brashi, rangi n.k. uchongaji huhitaji mundu, gogo, tupa, n.k. Uzuri wa umbo na sanaa za ufundi upo katika kuona. Sanaa hii hailazimishi fanani na hadhira kuwepo mahali pamoja kwa wakati mmoja. c) Sanaa za maonesho Ni kazi mbalimbali za Sanaa ambazo hutegemea utendaji (mfa...
MAENDELEO YA FASIHI SIMULIZI UWASILISHAJI NA UENEZAJI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI FASIHI SIMULIZI: Fasihi simulizi ni sanaa ambayo hutumia mazungumzo na matendo katika kuwasilisha ujumbe Fulani kwa watazamaji au wasikilizaji. Mazungumzo hayo huweza kuwa ya kuimbwa kutendwa au kuzungumzwa, Aina hii ya fasihi imepokelewa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo. Msimulizi katika fasihi simulizi mbali na kutumia mdomo wake hutumia viungo vyake vya mwili kama mikono, miguu, ishara mbalimbali katika uso wake na hata kupandisha na kushusha sauti yake. Kwa ujumla anaweza kutumia mwili wake mzima katika kuwasilisha na kufanikisha ujumbe wake kwa hadhira yake ambayo huwa ana kwa ana. Isotoshe anafaulu katika kutoa picha halisi ya dhana anayotaka kuiwasilisha kama ni ya huzuni, furaha, kuchekesha n.k. Zaidi ya kusimulia, kuimba na kuigiza msanii wa fasihi simulizi huwa na nafasi ya kushirikisha hadhira yake kama wahusika katika sanaa yake. Anaweza kutimiza hayo kwa kumfanya mshiri...
MAENDELEO YA KISWAHILI ASILI YA LUGHA YA KISWAHILI Neno asili lina maana kuwa jinsi kitu au jambo lilivyotokea au lilivyoanza na tunapozungumzia asili ya lugha ya Kiswahili ina maanisha tunachunguza namna lugha hiyo ilivyoanza. Wataalamu mbalimbali wa lugha wamefanya uchunguzi juu ya asili ya lugha ya Kiswahili. Uchunguzi huo umejenga nadharia mbalimbali zinazoelezea chimbuko la lugha ya Kiswahili. Kwa ujumla historia kuhusu asili ya lugha ya Kiswahili ina matatizo mengi na ndiyo maana kuna nadharia mbalimbali zinazoelezea juu ya asili ya lugha ya Kiswahili. Miongoni mwa matatizo yanayoikabili historia ya Kiswahili ni pamoja na: Hakuna uthibitisho kamili juu ya nadharia zinaelezea asili ya lugha ya Kiswahili na kuenea kwake. Uchunguzi wa asili ya Kiswahili ulifanywa na wataalamu wa kizungu ambao waliandika historia ya Kiswahili jinsi walivyoelewa wao baada ya kupata ushahidi kidogo tu. Wazawa hawakushirikishwa ipasavyo katika uchunguzi wa lugha ya Kiswahili. Hapakuwa na k...
VIAMBISHI Baadhi ya watu huchanganya dhana ya viambishi na dhana ya mofimu. Lakini ukweli ni kwamba mofimu na viambishi ni dhana mbili tofauti zenye mabwiano Fulani pia. Kwa ujumla viambishi vyote ni mofimu na mofimu zote ni viambishi SWALI: VIAMBISHI NI NINI? Viambishi ni mofimu zinazoandikwa kwenye mizizi wa neno ili kukamilisha muundo wa neno husika. Katika lugha ya Kiswahili viambishi vinaweza kuandikwa kabla ya mzizi wa neno na baada ya mzizi wa neno. kwa hiyo katika lugha ya kiswahili viambishi hutokea kabla ya mzizi wa neno na baada ya mzizi wa neno AINA ZA VIAMBISHI Lugha ya Kiswahili ina viambishi vya aina mbili VIAMBISHI AWALI/TANGULIZI Hivi ni viambishi ambavyo hutokea mwanzoni mwa mzizi wa neno na huwa ni vya aina mbalimbali A.Viambishi idadi /ngeli Viambishi hivi hupatikana mwanzoni mwa majina vivumishi kwa lengo la kuonesha idadi yaani wingi na umoja, Mfano : M – cheshi wa –zuri M – tu wa - tu Ki – ti vi-ti ...
UTUMIZI WA LUGHA Matumizi ya lugha ni namna yakutumia lugha kulingana na mila, desturi na taratibu zilizopo katika jamii husika. Ni jinsi ambavyo mzungumzaji anatunza lugha kwa kuzingatia uhusiano wake na yule anayezungumza naye. Matumizi ya lugha hutegemea mambo kadhaa Kama vile: Uhusiano baina ya wazungumzaji. -Mada inayozungumzwa -Mazingira waliyomo wazungumzaji n.k Umuhimu wa matumizi ya lugha Kuwasaidia watumiaji wa lugha kutumia lugha kwa ufasaha Kumsadia mzungumzaji kuweza kutambua kutofautiana na kutumia mitindo mbalimbali ya lugha MTINDO WA LUGHA Mtindo wa lugha ni mabadiliko yanayojitokeza katika kutumia lugha mabadiliko ya lugha katika mitindo mbalimbali yaani mitindo mbalimbali ya lugha. Kwa kawaida mtindo wa lugha / mabadiliko katika kutumia lugha ndiyo inayomwongoza mzungumzaji katika kuelewa maneno na mitindo ya tungo, Matumizi katika lugha hutawaliwa na mambo ya...
MATUMIZI YA SARUFI NADHARIA ZA SARUFI Dhana ya sarufi ya lugha imefafanuliwa na wataalamu mbalimbali wa sarufi. Mtaalamu James Salehe Mdee (1999) sarufi ya Kiswahili sekondari na vyuo anafafanua maana ya sarufi kuwa ni mfumo wa kanuni za lugha zinazomwezesha mzungumzaji kutunga sentensi sahihi na zenye kukubaliwa na wazawa wa lugha. Kanuni hizi hujitokeza katika lugha ya mzawa wa lugha inayohusika ambaye anaifahamu barabara lugha yake. Sarufi inajumuisha mfumo wa sauti maumbo ya maneno muundo na maana. Mtaalamu Mbundo Msokile (1992) na khamisi (1978) wanasema sarufi ni mfumo wa taratibu na kanuni zinazotawala matumizi sahihi ya matamshi, maumbo ya maneno, miundo ya tungo na maanda ya miundo ya lugha. Ni mfumo wa taratibu zinazomwezesha mzungumzaji wa lugha kutoa tungo sahihi na pia inamwezesha mtu yeyote anayezungumza kuelewa tungo zinazotolewa na mtu mwingine anayetuma lugha hiyo hiyo. F. Nkwera (1978) anasema sarufi ni utaratibu wa kanuni zinazomwezesha mzawa au mtumiaji ...
NOMINO /MAJINA (N) Majina ni aina ya maneno ambayo hutaja vitu, viumbe, hali au matendo ili kuviainisha na kuvitofautisha na vitu vingine. Mfano: Winnie, Werevu, Wema, Lulu, Mtu, Ubungo, Mungu na n.k AINA ZA MAJINA a.Majina ya kawaida Majina haya yanataja viumbe kama vile wanyama, miti, watu, ndege, wadudu. Majina yote hayo yanapoandikwa huanza kwa herufi ndogo kama yanatokea katikati ya sentensi au tungo. N:B Majina hayo sio maalumu kwa vitu Fulani tu bali kwa vitu mbalimbali. b. Majina ya Pekee. Haya ni majina maalumu kwa watu au mahali ambaye huonesha upekee kwa watu,mahali au vitu, Majina haya hujumuisha majina binafsi ya watu na majina ya mahali. Mfano: Marcus, Halima, James, Abel, Fredy, Anna Ubungo, Manzese, Tanzania, Uingereza, Africa N: B Majina hayo yanapoandikwa huanza kwa herufi kubwa C. Majina ya jamii. Haya ni majina ambayo yanataja vitu au watu wakiwa katika makundi au mafungu japo huwa majina hayo yapo katika hali ya umoja. Mfano,...
KUBAINISHA MOFIMU Kubainisha mofimu ni kuligawa neno katika mofimu zinazolijenga neno na kueleza kazi za kila mofimu ubabaishaji huo wa mofimu hufuata hatua zifuatazo 1. Kutambua aina ya neno – Yaani kama neno hilo ni tegemezi au neno changamano, Neno huru huundwa na mofimu huru na neno tegemezi huundwa na mofimu tegemezi na neno changamano huundwa na moja huru na mengine tegemezi N: B Neno huru huwa halivunjwi vunjwi kwani huundwa na mofimu huru 2. Kulitenga neno na kulivunja vunja katika mofimu zinazojenga neno hilo yaani hujenga mofimu awali, mzizi na mofimu tamati. N: B Mofimu awali, mzizi na mofimu tamati hupatikana katika maneno tegemezi na maneno changamano 3. Kueleza kazi ya kila mofimu Mfano: Bainisha mofimu katika maneno yafuatayo Hatukupendi Hili ni neno tegemezi ii. 1- Mofimu awali kianzishi, nafsi ya kwanza wingi 2 - Mofimu awali rejeshi kwa mtendwa 3 - Mofimu awali rejeshi kwa mtenda 4 - Mofimu mzizi 5 ...
UTUNGAJI Maana ya utungaji Utungaji ni pato la akili ya mtu binafsi ambayo hurejeshwa kwa fani kama vile macho, ushairi, tamthiliya au hadithi. Utungaji ni kitendo cha kuyatoa mawazo ubongoni, kuyakusanya na kisha kuyadhihirisha kwa kuyaandika au kuyazungumza. Ni kitendo cha kuunda hoja na kuyapanga katika mtiririko unaofaa katika lugha kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii husika. SIFA ZA MTUNGAJI Mtunzi analazimika kuelewa kikamilifu mada inayoshughulikiwa. Mtungaji lazima azingatie kanuni na taratibu za uandishi. Mtungaji anatakiwa kuzingatia mpango mzuri na wenye mantiki wa mawazo kutoka mwanzoni hadi mwishoni. Mtungaji anapaswa kuwa na msamiati wa kutosha ili kumwezesha kutumia lugha bora, sanifu, na fasaha. Mtunzi anapaswa kuzingatia sarufi ya lugha anayoitumia. Mtunzi anapaswa kujali nyakati zinazofaa. Mtunzi anapaswa kuwa na uwezo wa kutosha wa kuhusisha yanayoelezwa na hali halisi ilivyo katika j...