VIAMBISHI
Baadhi ya watu huchanganya dhana ya viambishi na dhana ya mofimu. Lakini ukweli ni kwamba mofimu na viambishi ni dhana mbili tofauti zenye mabwiano Fulani pia. Kwa ujumla viambishi vyote ni mofimu na mofimu zote ni viambishi
SWALI: VIAMBISHI NI NINI?
Viambishi ni mofimu zinazoandikwa kwenye mizizi wa neno ili kukamilisha muundo wa neno husika. Katika lugha ya Kiswahili viambishi vinaweza kuandikwa kabla ya mzizi wa neno na baada ya mzizi wa neno.
kwa hiyo katika lugha ya kiswahili viambishi hutokea kabla ya mzizi wa neno na baada ya mzizi wa neno
AINA ZA VIAMBISHI
Lugha ya Kiswahili ina viambishi vya aina mbili
VIAMBISHI AWALI/TANGULIZI
Hivi ni viambishi ambavyo hutokea mwanzoni mwa mzizi wa neno na huwa ni vya aina mbalimbali
A.Viambishi idadi /ngeli
Viambishi hivi hupatikana mwanzoni mwa majina vivumishi kwa lengo la kuonesha idadi yaani wingi na umoja, Mfano :
M – cheshi wa –zuri
M – tu wa - tu
Ki – ti vi-ti
m- ti mi - ti
N:B Wakati mwingine katika majina na vivumishi huweza kuandikwa, viambishi ambavyo hudokeza ukubwa wa nomino na vivumishi. Hivyo wakati mwingine majina na vivumishi huandikwa viambishi ambavyo hudondokea udogo wa majina na vivumishi.
Mfano: ji – tu ma – jitu
Ju –mba ma – jumba
Ki - toto vitoto
Ki –vulana vi – vulana
Ki – zuri vi – zuri
B. Viambishi awali vya ukanushi
Viambishi vya ukanushi kwa kawaida huwekwa mwanzoni mwa vitenzi ili kukanusha vitenzi husika. Viambishi ambavyo huandikwa katika vitenzi vya lugha ya Kiswahili ili kuonesha ukanushi wa tendo ni viambishi,
“Si” “ha” na “bu”
Kiambishi “ha” hutumika kukanzisha kitenzi kilichofanywa na nafsi ya kwanza wingi nafsi ya pili wingi na nafsi ya tatu katika umoja na wingi. Katika nafsi ya pili hutumika alomofu “ku” ambayo hukanusha nafsi ya pili umoja
Mfano: ni - na --- imba ---si ---imbi
U – na – imba – hu – imbi
Tu - na –imba --- ha –tu --- imbi
m- na – imba – ha -- mu--- imbi
wa ---na – imba --- ha ---wa –imbi
C. Viambishi vipatanishi / nafsi
Hivi ni viambishi ambavyo huwekwa kabla ya mzizi wa kitenzi na kubadilika kutegemeana na aina ya neno linalopatanishwa na kitenzi husika, kazi ya viambishi hivi ni kuonesha nafsi.
Mfano;
Ni – nasoma tunasoma
A - nasoma m – mnasoma
U- nasoma wa – nasoma
Viambishi vya njeo /wakati
Kiambishi cha njeo ni kiambishi ambacho huwekwa katika kitenzi ili kuwakilisha muda ambapo tendo husika limetendeka. Mfano tendo kama limefanyika wakati uliopita huwakilishwa na kiambishi (-li-) katika uyakinishi na kiambishi (-ku) tendo hilo linapokanushwa
Ni- li—soma Si – ku - soma
U – li- soma hu – ku - soma
A – li- soma ha – ku-soma
Tu – li – soma hatu-ku-soma
M-li – soma ham-ku-soma
Wa – li- soma hawa-ku-soma
Viambishi vya hali
Hivi ni viambishi ambavyo huwekwa kabla ya mzizi ambavyo hutumika kuonesha muda au kipindi maalum ambao tendo, lilifanyika viambishi vya hali hueleza kama tendo linaendelea kufanyika kama hufanyika mara kwa mara kama limemalizika kufanyika
Hali ya kuendelea kwa tendo
Hali ya kuendelea kwa tendo huwakilishwa na kiambishi (-na-) ambacho huwekwa kabla ya mzizi wa kitenzi
Mfano ni - na – imba
Tu – na-imba
U-na-imba
M-na-imba
A-na-imba
Wa-na-imba
Hali timilifu
Hali hii huwakilishwa na kiambishi”me” katika uyakinishi na kiambishi “ja” katika ukanushi. Mfano:
Ni – na-soma Si – ja- soma
Tu-me-soma hatu-ja-soma
M-me-soma ham-ja-soma
A-me-soma ha-ja-soma
Wa-me-soma hawa – ja-soma
Hali ya mazoea
Hali ya mazoea huwakilishwa na kiambishi (-hu-)
Mfano: hu – soma
hu – imba
hu –cheza
hu – cheza
hu- lala
Hali ya masharti
Hali ya masharti huwakilishwa na viambishi (-ki-) (-nge-)
Mfano: kiambishi (-ki-) hudokeza uwezekano
Tu- Ki-shinda – tukishinda tutafurahi
A-ki-ja – akija nitamwambia
Kiambishi (-nge-) hudokeza matumaini kidogo
A-nge-nilipa-Juma pesa yangu ningenunua gari.
Kiambishi (-ngali-) hudokeza kutokua na matumaini yeyote au kuwepo kwa matumaini kidogo kuliko yale yanayodokezwa na kiambishi (-nge-); mfano ningalijua kua nitafeli mtihani ningalisoma kwa bidii.
Viambishi vya mtenda
Hivi ni viambishi ambavyo hurejesha tendo kwa nomino ya mtenda, viambishi hivi hutegemea aina ya nomino inayorejeshewa
Mfano: ali – ye – piga
Uli-o-vuna
Vili-vyo-anguka
g.Viambishi vya urejeshi kwa mtendwa (yambwa)
Hivi ni viambishi ambavyo hurejesha tendo kwa nomino ya mtendwa wa jambo
Mfano: ali – ye-pigwa
Ali – o- vunjwa
Vili – vyo – angushwa
h. Viambishi virejeshi kwa mtendewa (kiambishi yambiwa)
Hivi ni viambishi ambavyo hurejesha tendo kwa nomino ya mtendwa jambo
Mfano: ali – ye-somewa
Viambishi vya urejeshi wa kujitendea
Hivi ni viambishi ambavyo hutokea kabla ya mzizi wa kitenzi na huwakilishwa na kiambishi (-ji-) ya kujitendea ambavyo hutumika katika umoja na wingi na pia katika uyakinishi na ukanushi
Mfano: nili – ji-somea siku – ji- somea
Nime- ji-kata sija-ji-kata
Nina-ji-somea si – ji-somei
Ana-ji-somea ha-ji-somei
Una-ji-somea ha-ji-somei
Tun-ji-somea hatu-ji-somei
Tuta-ji-somea hatuta-ji-somea
Mta-ji-somea hamta-ji-somea
Wali-ji-somea hawaku-ji-somea
VIAMBISHI KATI
Viambishi kati ni viambishi ambavyo hupachikwa ndani ya mzizi wa neno na hivyo kuukata mzizi katika sehemu kuu mbili (2)
N.B; Viambishi kati huwepo katika lugha ya Kiswahili kwa sababu maneno ya lugha ya Kiswahili kwa tabia yake hawaruhusu upachikaji wa viambishi kati ya mzizi, viambishi hivi hutokea katika lugha nyingine mfano kiebrania.
VIAMBISHI TAMATI
Hivi ni viambishi ambavyo huiweka baada ya mzizi wa neno. Navyo ni vya aina kuu mbili (2)
(a) Viambishi tamati maana
(b) Viambishi tamati vijenzi
Viambishi tamati maana
Viambishi tamati maana ni viambishi ambavyo hukamilisha maana ya neno. Viambishi hivi huwa haviadhiri maana ya awali ya neno yaani havijengi dhana mpya katika neno
Mfano: a-na-som-a
Tend –a
Kata –a
Kat –a
Viambishi tamati vijenzi
Hivi ni viambishi ambavyo hujitokeza mwishoni mwa mzizi wa neno ili kujenga dhana mpya
Mfano: piga – pig -o
Mcheza – Mcheza-ji
Soma – som -a
Viambishi tamati hufanya kazi mbalimbali kama vile kudokeza kauli mbalimbali za vitenzi
i. Kauli ya kutenda
Hii ni kauli ambayo hueleza jambo lililotendwa na mtenda. Viambishi ambavyo hubainisha kauli ya kutenda ni viambishi tamati maana ambavyo huwa ni vimalizio vya mzizi wa kitenzi
Mfano gand – a
Pig – a
Som –a
ii.Kauli ya kutendwa
Kauli hii hueleza kuwa mtu, watu au vitu Fulani vimetendwa jambo Fulani, Alomofu ambazo huwakilisha kauli ya kutendwa ni (-wa) (-liw) (-lew-)
Mfano: pig – w-a
Sem – w-a
Chom- w-a
O – lew – a
Vu – liw – a
Ambi – w-a
iii.Kauli ya kutendewa
Kauli hii huonesha kuwa mtu Fulani ametenda kwa niaba ya mtu mwingine, Alomofu ambazo hutumiwa kuonesha kauli ya kutendewa ni (-iw-), (ew-) (-liw-) (-lew-)
Mfano: lim – iw-a
Chez-ew-a
Som-ew-a
Kimbi-liw-a
Zo-lew-a
Va-liw-a
Chomo-lew-a
IV. Kauli ya kutendea
Kauli hii huonesha kuwa tendo limefanyika kwa manufaa, kwa niaba au kwa faida ya mtu mwingine alomofu za kauli ya kutendea ni (i) (-e-) (-li-) (-)
Mfano: pig – i-a
Lal – i-a
Ruk-i-a
Chez-e-a
Zo-le-a
o-le-a
V. Kauli ya kutendesha
Kauli hii huonesha wababaishaji ambao huwezakuwa na mhusika au wahusika Fulani wanaosababisha kufanyika kwa tendo la mhusika na wahusika wengine. Kauli hii huonesha mtu fulani wanavyosababisha kufanyika kwa tendo kwa mhusika na wahusika wengine. Kauli hii huonesha mtu Fulani anamsababishia mtu mwingine kufanya jambo Fulani za utendaji (-ish) (esh-) (-lish) (-lesh-) (sh) na (-z)
Mfano : imb – ish –a
Kimbi – z –a
Tembe – z-a
Pit – ish –a
ru – sh –a
VI. kauli ya kutendesha (usababishaji)
Ni kauli ya wasababishi ambao huwezakuwa ama mhusika au wahusika Fulani wanaosababisha kufanyika kwa tendo kwa mhusika au wahusika wengine. Kauli hii huonesha mtu fulani ana msababisha mtu mwingine kufanya jambo Fulani.
Og – esh –a
Zo-lesh-a
Ka-lish – a
Va-lish-a
Shon-esh-a
Som-esh-a
Chem-sh -a
Vii. Kauli ya kutendana
Kauli hii huonesha wahusika Fulani kuhusika na tendo Fulani ambapo mhusika wa kwanza anamtenda mhusika wa pili, lakini pia mhusika wa pili ana mtendea mhusika wa kwanza katika jambo hilo hilo.
Adhari ya tendo linalofanyika huwa kwa pande zote mbili yaani mtu wa kwanza na mtu wa pili. Kauli hii hudhihirishwa na kiambishi (-an-) ambacho hutokea baada ya mzizi wa kitenzi.
Mfano: pend – an-a
Suk – an –a
Sukum – an –a
Sem – an – a
Ruki – an –a
Viii. Kauli ya kutendeana
Kauli hii huhusisha tendo linalofanywa na watu wawili ambapo mhusika wa kwanza anafanya tendo Fulani wka mambo ya mhusika wa pili na muhusika wa pili anafanya tendo hilo hilo kwa niaba ya muhusika wa kwanza. Kiambishi kinachodhihirisha kauli hii ni (-an-) ambayo hutokea kati ya kiambishi kinachofuata baada ya mzizi wa kitenzi na kiambishi tamati maana
Mfano: suk – i – an –a
Sem-e-an-a
Som-e-an –a
Zo-le-an-a
Va-li-an-a
O-le-an-a
ix. Kauli ya kutendana (kufungamana)
Hili ni kauli ambayo hurejelea hali, ambapo watu au kitu hukaa pamoja kwa muda mrefu. Mofimu ya kauli hii katika lugha ya Kiswahili ni (-am-) ambayo hujitokeza katika vitenzi vichache
Ung – am-a
Ach – am –a
x. Kauli ya kutendwa
Hi ni kauli ambayo huonesha kinyume cha tendo. Na kauli hii hudhihirishwa na kiambishi (-o) na (-u-)
Mfano: umb – u –a
Teg – u – a
Chom – o –a
Kunj – u-a
Pang – u –a
Xi Kauli ya kutendana (kishikanishi)
Hii ni kauli inayoonesha mshikamano yaani tendo la kufanya watu au vitu kushikana na mofimu inayodhihirisha kauli hi ni (-at-)
Mfano:Pak-at-a
Kam-at-a
Fumb – at – a
SHINA NA MZIZI
Mzizi /kiini ni sehemu ya neno inayobakia baada ya kuondoa aina zote za viambishi yaani viambishi vya awali vyote na viambishi tamati vyote.
Mzizi ni sehemu ya muhimu ambayo hubeba maana ya msingi katika neno
AINA YA MZIZI
Kuna aina kuu mbili (2) za mzizi
Mzizi fungo/tegemezi
Huu ni mzizi ambao hauwezi kujitegemea yaani huwezikusimama peke yake kama neno na kuleta maana
Mfano: som — a
Chom – a
Pend -a
(a) (chom-), ( som) na (pend-) ni mzizi tegemezi ambayo haiwezi kusimama yenyewe bila kuleta maana
Mzizi huru/sahihi
Huu ni mzizi ambao unaweza kusimama peke yake kama neno na kuleta maana.
Mfano: Jembe
Ng’ombe
Winnie
Marcus
Abel
Concepta
Shina ni nini?
Shina ni sehemu ya neno (mzizi asilimia waneno) ambayo hufungamanishwana irabu mwishoni isiyokuwa na maana maalum kisaruji
Mfano: Neno shina
Mtoto toto
Wanacheza Cheza
AINA ZA MASHINA
Shina sahili /huru
Hili ni shina ambalo huundwa na mofimu moja tu ambayo pia huwa ni mzizi wa neno. Mfano ng’ombe, kuni, tafiti
Shina changamano
Ni shina ambalo huundwa na mzizi pamoja na kiambisi mwishoni, Mfano cheza soma, na kimbia.
Shina ambatani/ ambatana
Hili ni shina ambalo linaundwa na mofimu mbili ambazo zote huwa ni mzizi
Mfano: mwana + nchi
Pima + Maji
NB: Katika lugha ya Kiswahili wakati mwingine hulingana na mzizi na mofimu. Kulingana kwa dhana hizo hakuna maana kwamba dhana hizo ni sawa.
DHANA YA MOFU
Dhana ya mofu inafafanuliwa na wataalamu mbalimbali wa sarufi kama ifuatavyo;
Mtaalamu (Nick 1949) anafafanua mofu kuwa ni umbo la neno ambalo huwakilisha mofimu na ambalo hudhihirika kifonolojia na kiothografia.
Mofimu ambazo elementi dhahania, huwakilishwa na mofu ambazo hudhihirika kifanolojia zikiwa na sauti za kutamkwa, au kiothografia zikiwa ni alama za kuandikwa.
TUKI (1990) wanafafanua kuwa mofu ni kipashio cha kimofolojia kiwakilichasho mofimu
marealle (1978) anafafanua kuwa mofu ni vipande vya neno ambavyo husitiri mofimu. Kila mofu inamaana Fulani, Vipande hivyo vya maneno huwa na maana maalum katika kila neno hutegemeana na jinsi lilivyotumia.
N.B: Kutokana na maana hizo tatu za mofu tunapata mambo ya msingi kabisa ambayo hutumika kupambanua na dhana ya mofu. Pia kutokana na maana hizi tatu tunapata sifa za msingi zinazotumika kupambanua dhana ya mofu.
SIFA ZA MOFU
Mofu ni sehemu halisi ya neno
Mofu ni maumbo halisi ya maneno ambayo hutamkwa na watu wanapozungumza au kuandikwa, Kwa hiyo mofu ni umbo halisi ambalo linaweza kusikika linapotamkwa na linaweza kuonekana kwa macho ijapokua limeandikwa.
Mofu hudhihirika kifonolojia na kiathografia
Mofu ni umbo halisi la neno na kwa kuwani ni umbo halisi la neno basi mofu hudhihirika kifonolojia zinapotamkwa na kimaandishi zinapoandikwa.
Mofu huwakilisha maana
Kila mofu huwakilisha maana Fulani, Neno lolote lile katika lugha yoyote ile litakuwa na maana,
Maana hiyo huwa imesitiriwa katika mofu zinazolijenga neno hilo.
Hii ina maana kuwa kila neno lenye maana Fulani lazima maana hiyo itakuwa imewakilishwa na mofu Fulani. Pia hakuna neno lolote katika lugha yoyote ambalo litakauwa ni neno lenye maana bila kuwa na mofu angalau moja.
Mofu ni kipashio kidogo kabisa cha neno
Mofu ndiyo sehemu ndogo kabisa katika neno ambayo hubeba maana na sehemu hiyo haiwezi kugawanyika katika sehemu ndogo zaidi zilizo na maana. Mofu ni umbo ambalo ni kubwa kuliko fonimu lakini ni dogo katika neno.
N.B: Lakini katika lugha ya Kiswahili wakati mwingine mofu hulingana na neno. Mofu ni vile viambishi mbalimbali ambavyo huwa vinawekwa kwenye mzizi wa neno pamoja na mzizi wenyewe. Kila kiambishi cha neno pamoja na mzizi wenyewe.Kila kiambishi cha neno ni mofu na mzizi wa neno pia ni mofu. Mfano:
Mofu huainishwa kwa kutumia vigezo vikuu viwili
Kigezo cha maana yaani maana zinazowakilishwa mofu
Kigezo cha mofolojia ya mofu
Kwa kutumia kigezo cha maana kuna aina tatu (3) za mofu
Mofu huru
Mofu funge
Mofu tata
Kwa kutumia kigezo cha mofolojia kuna aina kuu tatu (3) za mofu
Mofu changamano
Mofu funge
Mofu tata
Kwa kutumia kigezo cha mofolojia kuna aina kuu tatu (3) za mofu
Mofu changamano
Mofu mzizi
Mofu kopa
MOFU HURU
Mofu huru ni mofu ambazo zinaweza kukaa zenyewe kama maneno yenye maana inayoeleweka bila kusaidiwa na mofu nyingine,
Mfano: Nomino (kaka) (paka) sungura)
Vivumishi (safi) (udhaifu)(hodari) Imara) Zuri
Vielezi ((Haraka) (Juzi) Leo
Vitenzi (afiti) Samohe) Ariful)
Viunganishi (halafu) (pia) (ila)
II. MOFU FUNGE
Hizi ni mofu ambazo haziwezi kutumika peke yake kama neno kamili bali hutumika kama kiambishi ambacho huambatana na mofu nyingine ili kukamilisha neno
Mofu funge inasifa mahususi
Haiwezi kusimama peke yake ikajitegemea kwa kawaida
Kwa kawaida mofu funge ni mofu tegemezi hivyo ni lazima iambatane na angalau mofu nyingine moja ili iweze kujitosheleza kimaana. Baadhi ya wanaisimu huiita mofu tegemezi
Maana ya mofu funge hutegemea muktadha wa mofu kimahusiano na mofu nyingine. Mofu tegemezi kazi zake huwa zimefungwa kwenye muktadha maalumu na zinapoondolewa kwenye muktadha huo hukosa maana na ni vigumu kujua bila kuweka katika muktadha wa neno.
Mfano; Kula – (ku) + (l) + (a)
Kunjwa – (ku) (nyw) + (a)
Mpe – (m) + (pe)
Sikusoma – (si) + (ku) + (som) +(a)
Mofu hizi ni mofu tegemezi kwa sababu haziwi wazi kusimama zenyewe
III. MOFU TATA
Hizi ni mofu ambazo huwa na maana zaidi ya moja na hivyo husababisha tungo kueleweka kwa namna zaidi ya moja
Mfano: Juma alimpiga John mpira
Juma alimpiga mpira kwa kuelekezakwa John
Juma alitumia mpira kama kifaa cha kumpigia Johari
Juma alipiga mpira kwa niaba ya John
Juma alimpiga John kwa sababu ya mpira
Maana hizi nne zimesababishwa na mofimu tata (-i-) Ambayo inajitokezakatika sentensi alimpigia
IV MOFU CHANGAMANO
Hizi ni mofu ambazo huundwa angalau na mashina au mizizi miwili ya neno ambayo katika mazingira na kila mmoja hujitegemea,
Mfano: Kiona mbali Mofolojia ya neno hili ina uweo kutazamwa kwa namna kuu mbili
Namna ya kwanza: linaweza kutazamwa kama neno lenye mofu tatu (3)
(ki-) + (on-) + (-a-) + (mbali)
Linaweza kutazamwa kama neno lenye mofu tatu (3)
(ki-) + (-on-) + (-mbali-)
(ki-) + (-onambali)
Katika neno kuona mbali kuna mizizi miwili, linaweza kutazamwa kama neno moja lenye mzizi mmoja
(-onambali) hii ni mofu changamano kwa sababu huundwa na mizizi miwili ambayo katika mazingira mengine inaweza kutenganishwa na kila mzizi kujitenga enyewe.
V. MOFU KAPA
Hizi ni mofu za kipekee ambazo hazina umbo hazitamkwi tunapozungumza wala haziandikiwi tunapoandika, wala hazionekani kabisa katika neno lakini athari za nafuu hizo huwa miongoni mwa wazungumzaji.
NB: Ingawa mofu kapa hazitamkwi wala kuandikwa, hazisikiki wala kuonekan kwa macho lakini maana zake huwa zipo na tunazipata zinapotumika katika maneno ; kwa mfano tukichunguza maumbo ya umoja na wingi katika majina ya Kiswahili, Majina hayo yanaweza yakagawanywa katika makundi mawili (2)
Ni majina yenye maumbo dhahiri ya umoja na wingi
Mfano m – pira mi – pira
m-ti mi –ti
ki – ti vi – ti
ALOMOFU.
Alomofu ni maumbo zaidi au maumbo tofauti ambayo huwakilisha mofimu moja kisarufi ambayo hufanya kazi moja kisarufi, alomofu hutokea mazingira maalum baadhi ya mazingira hutabirika mengine hayatabiriki kabisa. Alomofu kwa kawaida hubadili maana ya neno.
UTOKEAJI WA ALOMOFU
Mazingira ya kifonolojia (matamshi)
Mfano: Mtu anaposikia neno “funguo” anajua ni zaidi ya moja.
vi. MOFU MZIZI
Mofu mzizi ni kiini cha neno. Mofu mzizi ndio hubeba maana ya msingi katika neno. Mofu huwa haibadiliki neno linapoandikwa mofu nyingine
Mfano;(u) +(Funguo) na (wa) + (toto)
Funguo na toto ni mofu mzizi
N:B Uainishaji wa aina hizo za mofu huzingatia maana zinawakilishwa na mofu na kigezo kwa kigezo cha kimofolojia.
TUNGO
Neno tungo hutokana na kitenzi tunga, Wanasema hufasiri kuwa tungo ni matokeo ya kuweka na kupanga pamoja vipashio vidogo ili kujenga vipashio vikubwa zaidi katika lugha. Katika sarufi tungo ndogo kuliko tungo nyingine za neno ambalo huundwa kutokana na kuwekwa pamoja mofimu kuwa tungo kubwa kuliko nyingine zote ni tungo.
AINA ZA TUNGO
Katika lugha ya Kiswahili kuna aina kuu nne za tungo ambazo huainishaji wake au mpangilio wake unazingatia hali ya tungo. Tungo hizo hupangwa kuanzia tungo ndogo hadi kubwa zaidi,
1. Tungo neno ambayo hujengwa na mofimu
2. Tungo kirai ambayo hujengwa na maneno
3. Tungo kishazi ambayo hujengwa na maneno au kirai
4. Tungo sentensi ambayo hujengwa na tungo kirai au kishazi
1. TUNGO NENO
Neno ni mkusanyiko wa silabi , au silabi hutamkwa au huandikiwa na kuleta maana
Mfano: Ng’ombe
Tafiti
Anatembea
Taifa
N:B : Neno hujengwa na mofimu moja au zaidi, Neno linalojengwa na mofimu moja huitwa neno sahili au huru na neno linalojengwa na mofimi zaidi ya moja huitwa neno changamoto. Maneno mengi katika lugha ya Kiswahili ni changamana,
AINA ZA MANENO
Wataalamu wa lugha ya Kiswahili wanatofautiana katika uainishaji wa aina za maneno. Wapo ambao wanaainisha aina saba (7) tu za maneno katika lugha ya Kiswahili na wengine huainisha aina nane (8) za aina za maneno. Wataalamu wanoainisha aina saba za maneno F. Mkwera (1978), Kapinga (1983) TUMI (1988) Mohamed (1986), Msamba na wanzake (1999) Kihore na wenzake (2001) wataalamu wengine wameainisha aina nane za maneno. MbundaMsokile (1992), J.S Mdee (1988), Ngullu R. (1999), Y. Rubanza (2003), MBadu (2000)
Wataalamu wanaoainisha aina nane za maneno hutofautisha dhana ya kiunganishi na kihisishi lakini wale wanaoainisha aina saba za maneno huona kuwa dhana hizo ni dhana mbili zinazofanana.