MATUMIZI YA SARUFI
NADHARIA ZA SARUFI
Dhana ya sarufi ya lugha imefafanuliwa na wataalamu mbalimbali wa sarufi.
Mtaalamu James Salehe Mdee (1999) sarufi ya Kiswahili sekondari na vyuo anafafanua maana ya sarufi kuwa ni mfumo wa kanuni za lugha zinazomwezesha mzungumzaji kutunga sentensi sahihi na zenye kukubaliwa na wazawa wa lugha. Kanuni hizi hujitokeza katika lugha ya mzawa wa lugha inayohusika ambaye anaifahamu barabara lugha yake. Sarufi inajumuisha mfumo wa sauti maumbo ya maneno muundo na maana.
Mtaalamu Mbundo Msokile (1992) na khamisi (1978) wanasema sarufi ni mfumo wa taratibu na kanuni zinazotawala matumizi sahihi ya matamshi, maumbo ya maneno, miundo ya tungo na maanda ya miundo ya lugha. Ni mfumo wa taratibu zinazomwezesha mzungumzaji wa lugha kutoa tungo sahihi na pia inamwezesha mtu yeyote anayezungumza kuelewa tungo zinazotolewa na mtu mwingine anayetuma lugha hiyo hiyo.
F. Nkwera (1978) anasema sarufi ni utaratibu wa kanuni zinazomwezesha mzawa au mtumiaji yeyote wa lugha kuelewa tungo zinazotolewa na mtu mwengine anayetunza lugha hiyo hiyo. Kufafanua nakuzielewa kwa undani tungo mbalimbali zitumikazo katika lugha hiyo pamoja na kutoa tungo sahihi na zinazoeleweka
HITIMISHO
Kwa ujumla maana zote zilizotolewa na wataalamu wote ni maana sahihi za sarufi ila tunaweza kuhitimisha kwa sarufi ni kanuni, sheria au taratibu zinazotawala lugha katika viwango yote vya uchambuzi wa lugha yaani kiwango cha sarufi matamshi (fonolojia) sarufi maumbo (mofolojia) sarufi miundo (sintaksia) na sarufi maana (semantiki)
AINA ZA SARUFI
Ujumla sarufi inaweza ikagawanywa katika aina kuu zifuatazo
SARUFI MATAMSHI (UMBO SAUTI)
Sauti katika lugha yaani jinsi ambavyo vitamkwa au sauti za lugha zinavyoungana ili kujenga maneno yanayokubalika katika lugha husika.
N.B: Sarufi matamshi hujishughulisha na uchambuzi wa sauti zilizomo katika lugha. Namna zinavyotamkwa, mahali zinapotamkwa na namna sauti hizo zinavyopangwa; ili kujenga maneno ya lugha Fulani.
Lugha mbili tofauti zinawezakuwa na sauti zinazofanana lakini zikatofautiana katika utaratibu wa kuzipanga sauti hizo. Kila lugha ina utaratibu wake wa mpangilio wa sauti ili kujenga ama mofimu, silabi au maneno. Sauti zitumikazo katika lugha zinaweza kugawanywa katika makundi mawili
i. Irabu, mfano a, e, i, o, u
ii. Kansonati, mfano k, g, ch, i, d
FONIMU
Fonimu ni kipashio kidogo kabisa cha kifonilojia ni kitamkwa cha msingi cha kifonolojia kinacho badili maana ya neno
K, P, B ni fonimu kwani ndio zinafanya maneno hayo kutofautiana kimaana.
T na g ni fonimu zinazofanya maneno haya kutofautiana kimaana.
Irabu na konsonanti zinapotumika katika luga huitwa alfabeti.
Irabu ni sauti za lugha ambazo hutamkwa bila kuwepo kwa kizuizi chochote kwenye mkondo wa hewa utokao mapafuni kwenda nje kupitia chemba ya kinywa na pua..
SIFA ZA IRABU
1. Irabu hutolewa kwa mrindimo wa ujenzi sauti
2. Irabu zinapotamkwa midomo ya mtamkaji huviringwa na kutandazwa
3. Utamkaji wa sauti hizi utegemea mkao wa ulimi katika chemba ya kinywa.
KONSONANTI
Ni sauti ambazo hutamkwa kwa kuzuia mkondo wa hewa katika sehemu mbalimbali kinywani hasa kwa kutumia ulimi.
i. Konsonanti ghuna: ni zile ambazo hutamkwa zikiwa na mrindimo mkubwa wa nyuzi sauti
ii. Konsonanti zisizosighuna(sighuna): ni zile ambazo hutamkwa zikiwa na mrindimo mdogo wa sauti
Katika Kiswahili sanifu, kuna konsonanti 23 na viyeyusho viwili hizo ni b, ch, d, dh, f, g gh, j, k, l, m, n, h, ny, ng, p, r, s, sh, t, th, v, z.
Na viyeyusha viwili ambavyo ni :
SILABI
Ni kitamkwa au sehemu ya neno ambayo hutamkwa mara moja na kwa pamoja kama sehemu ya fungu moja la sauti.
Silabi zinagawanyika katika makundi mawili
i. Silabi funge
ii. Silabi humo
i. SILABI FUNGE
Ni silabi zinazoishia na konsonanti
ii. SILABI HURU
Ni kitamkwa katika lugha (sauti katika luhga)
ALOFONI
Ni vitamkwa tofauti yaani sauti zinabadili maana ya neno. Mfano
Bh na b ni alafoni zinazobadili maana ya neno
2. SARUFI MAUMBO ( mofolojia)
Sarufi maumbo hujishughulisha na namna maneno ya aina mbalimbali yanavyoundwa katika lugha. Maneno katika lugha hujengwa kwa kuunganisha vipengele vidogo vya maneno ambavyo hubeba dhana mbalimbali kama vile nafsi,wakati,wingi,umoja, uyakinishi na kauli mbalimbali n.k
Vipande hivi vidogo vya maneno vijengavyo neno hufahamika kama mofimu, katika kila lugha kuna utaratibu wake wa kuzipanga mofimu ili kujenga maneno yenye maana katika lugha husika. Kwa kawaida mofimu hupangwa kwa kufuata utaratibu maalumu utarabu huo hujengwa kama utaratibu wa mpangilio kwa kufuata kanuni na huo utaratibu wa mpangilio wa mofimu usipofuata maumbo ya maneno yasiyokuwa na maana yaani yaliyokataliwa na wazawa wa lugha husika. Utaratibu wa kuzipanga mofimu ili kuzalisha maneno yenye maana katika lugha husika hutuzalia kanuni maumbo kwa mfano katika lugha ya Kiswahili mofimu za umoja na wingi katika nomino huwekwa mwanzoni katika utaratibu huu haukubaliki katika luhga ya kiingereza, katika lugha ya kiingereza mofimu za umoja na wingi huwekwa mwishoni mwa nomino. Mfano
Boy – boys
Girl – girls
Idea – ideas
N:B Kwa ujumla sarufi maumbo (mofolojia) hujishughulisha na jinsi ambavyo mofimu mbalimbali zinavyoungana ili kujenga maneno yatumikayo katika lugha. kipashio cha msingi katika mofolojia ya lugha ni mofimu.
3. SARUFI MIZINGO/UMBO TUNGO (Miundo maneno / sintaksia)
uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa maneno hayo sintaksia huchunguza sheria au kanuni zinazofuatwa katika kuyapanga maneno ya lugha yaani mpangilio wa neno moja baada ya jingine kwa namna ambayo itayafanya maneno hayo yalete maana inayokubalika katika lugha inayohusika wakati mwingine mpangilio wa maneno unaweza ukawa sahihi yaani ulizounda utaratibu lakini ukazalisha tungo zisizo kuwa na maana hiyo zitakuza mpangilio wa maneno wenye kuleta maana.
N:B Katika lugha ya Kiswahili kanuni kubwa ya kisintaksiani ni ile inayosema, kila sentensi iliyo sahihi na yenye kukubalika kwa wazao wa lugha ya Kiswahili sharti iwe na muundo wakiima na kiarifu au kikundi nomino na kikundi kitenzi.
4. SARUFI MAANA (UMBO MAANA SEMANTIKI)
Tawi hili la sarufi huchunguza maana inayoonekana wazi na maana iliyofichika huchunguza muundo wa tungo ili kupata maana iliyofichika. Katika lugha kila neno tungo huwa na maana yake. Kwa mfano, mtoto amelalia uji. Neno amelalia kama lilivyotumika, Katika sentensi hii halina maana moja na hivyo kuifanya sentensi hiyo kuwa na maana zaidi ya moja, mara nyingi maana ya neno hutegemea matumizi ya neno katika muktadha Fulani.
N.B.: Lugha inaweza ikafanya kazi sawasawa ambazo taratibu na kanuni za lugha husika zimefutwa. Taratibu hizo ni zile zinazohusu matamshi, maumbo, muundo na maana. Taratibu hizi ndizo humwezesha mzawa au mtumiaji yeyote wa lugha kutoa tungo sahihi na zinazoeleweka kwa matumizi mengine ya lugha na kuelewa tungo zinazokataliwa na watumiaji wengine wanaotumia lugha hiyo hiyo.
VIPASHIO VYA LUGHA
Lugha hujengwa na vipashio mbalimbali ambavyo vinatabia ya kujengana yaani vipashio vidogo huungana kujenga vipashio vikubwa zaidi.lugha ina vipashio vikuu vitano ambavyo ni
Mofimu - Neno - Kirai – Kishazi – Sentensi
Vipashio hivi wakati mwingine hufahamika kama tungo isipokuwa kipashio kidogo kwa vingine vyote katika lugha ni mofimu na kipashio kikubwa kuliko vingine vyote ni sentensi vipashio vyote katika lugha vina muundo maalum unaoonesha jinsi vinavyojenga vipashio vikubwa kuliko vingine vyote ni sentensi, vipashio vyote katika lugha vina muundo maalumu unaonekana jinsi vinavyojengwa isipokuwa mofimu
MOFIMU
Mofimu ndio kipashio cha msingi kinachoshughulika katika mofolojia ya lugha kwa maana mbalimbali za mofimu. Baadhi ya wataalamu hujaza mofimu kwa kutumia kigezo cha muundo wa mofimu na wengine hufasili kwa kutumia kigezo cha kazi au dhima zinazobebwa na mofimu husika.
MAANA YA MOFIMU
Mofimu ni sehemu ya neno au neno zima lenye maana ya kisarufi au maana ya kileksika
AU
Mofimu ni kipashio kidogo cha kimofolojia chenye kubeba maana iliyo ya kisarufi au ya kileksika
Mofimu hupangwa kwa kuzingatia utaratibu maalumu ili kujenga maneno yenye maana utaratibu huo hufahamika kama kanuni. Utaratibu wa upangaji wa mofimu ukikiukwa huzalisha maumbo yasiyokubalika katika lugha husika.
Mfano: a – na – som – a neno hili linakubalika katika lugha kwa sababu mpangilio wake wa mofimu umezingatia kanuni lakini mpangilio wake ungekuwa vinginevyo husingekuwa na maana
Mfano: som – na – a –a tungezalisha umbo lisilokuwa na maana. Kila lugha inautaratibu wake wa kuzipanga mofimu
N.B Wakati mwingine mofimu huwa na maana sawa na neno, mofimu hizo huitwa mofimu huru au mofimu za kilekisika. Mofimu hizi husimama zenyewe bila kutegemea mofimu nyingine na huwa na maana kamili.
AINA ZA MOFIMU
Mofimu zinaweza zikagawanywa katika makundi mawili kwa misingi ya kikazi yaani mofimu za kileksika na mofimu zakisarufi. Pia zinaweza kugawanywa katika makundi mawili kwa msingi wa kimuundo na kupata mofimu huru na mofimu tegemezi.
1. MOFIMU HURU (Mofimu sabili/mofimu za kileksika)
Hizi ni mofimu ambazo husimama zenyewe zinaumbo dogo zaidi bila kupoteza maana. Aina hiyo ya mofimu hujitokeza katika aina mbali mbali za maneno;
Mfano baba, Mama, kaka, na winnie ni nomino
-chafu, bovu, fupi, zuri na tamu ni vivumishi.
-Hata, lakini, kama, mpaka, au- viunganishi
-Arifu, tafiti, samehe- vitenzi
Mofimu zote huru huwa na kazi ya kileksika
2. MOFIMU TEGEMEZI
Hizi ni mofimu ambazo haziwezi kusimama ili kukamilisha dhana iliyokusudiwa. Mofimu tegemezi hujumuisha mofimu awali, mzizi, na mofimu tamati.Mpangilio wa
mofimu hizo au mfungamano wa mofimu hizo huunda neno. Mofimu hutumika katika kuunda maneno
N.B Mofimu tegemezi zinapofungana huunda neno tegemezi, mfano: a – na - som – a anasoma, nam – pend – a – nampenda
Mofimu huru huunda neno huru mfano, Baba, mama starehe, jaribu n.k Mfungamano wa mofimu huru na mofimu tegemezi hujenga neno changamano. Mfano; mw – ana – nchi
Mw – ana – anga