KUBAINISHA MOFIMU
Kubainisha mofimu ni kuligawa neno katika mofimu zinazolijenga neno na kueleza kazi za kila mofimu ubabaishaji huo wa mofimu hufuata hatua zifuatazo
1. Kutambua aina ya neno – Yaani kama neno hilo ni tegemezi au neno changamano, Neno huru huundwa na mofimu huru na neno tegemezi huundwa na mofimu tegemezi na neno changamano huundwa na moja huru na mengine tegemezi
N: B Neno huru huwa halivunjwi vunjwi kwani huundwa na mofimu huru
2. Kulitenga neno na kulivunja vunja katika mofimu zinazojenga neno hilo yaani hujenga mofimu awali, mzizi na mofimu tamati.
N: B Mofimu awali, mzizi na mofimu tamati hupatikana katika maneno tegemezi na maneno changamano
3. Kueleza kazi ya kila mofimu
Mfano: Bainisha mofimu katika maneno yafuatayo
Hatukupendi
Hili ni neno tegemezi
ii. 1- Mofimu awali kianzishi, nafsi ya kwanza wingi
2 - Mofimu awali rejeshi kwa mtendwa
3 - Mofimu awali rejeshi kwa mtenda
4 - Mofimu mzizi
5 - Mofimu tamati kanushi
6. Asiyekujua
i. Hili ni neno tegemezi
iii. 1. Mofimu awali nafsi ya tatu umoja
2. Mofimu awali kanushi nafsi ya tatu umoja wakati uliopo
3-Mofimu ya urejeshi kwa mtenda
4-Mofimu awali ya urejeshi kwa mtendwa
5-Mofimu mzizi
6. Mofimu tamati
C. Kikikitangulia
i. Hili ni neno tegemezi
ii 1. Mofimu awali nafsi ya tatu umoja
2. Mofimu awali kanushi ya nafsi ya tatu umoja wakati uliopo
3 Mofimu ya urejeshi kwa mtenda.
4. Mofimu mzizi
5. Mofimu tamati
5.
7.
d. Nimejikata
i. Hili ni neno tegemezi
ii 1 – Mofimu awali ya nafsi ya kwanza umoja
2 - Mofimu awali inayoonesha hali timilifu
3 – Mofimu awali ya urejeshi wa kujitendea
4 -Mofimu mzizi
5 -Mofimu tamati
e. Sipendeki
Hili ni neno tegemezi
-Si- pend - ek –i
1 2 3 4
1. - Si – mofimu awali kanushi nafsi ya kwanza umoja wakati uliopo.
2. - pend- mofimu mzizi
3. -ek- mofimu tamati ya kutendeka
4. -i- mofimu tamati ya ukanushi
DHIMA ZA MOFIMU
Mofimu huwa na dhima au kazi mbalimbali zinazotumika katika maneno.
Kazi za mofimu ni kama zifuatazo:-
1. Kuongeza msamiati katika lugha au kubadili maneno kutoka kategoria moja kwenda kategoria nyingine.
Mfano: Nyumba – Nyumbani
Soma – somo
Soma – msomi
Taifa - taifisha.
2. Kuongeza maana ya ziada au kupanua maana ya neno
Mfano: Taifa – Utaifa
3. Kudokeza dhana ya umoja na wingi
Mfano: Mtu – watu
iii. Ni majina yenye umbo la umoja lakini umbo la wingi hakuna
Mfano: Umoja Wingi
Ukuta Kuta
U – Funguo Funguo
U-Kucha Kucha
U-kope kope
iv. Ni maneno ambayo yana umbo dhahiri la wingi lakini umbo la umoja halipo
Mfano: Umoja Wingi
Ukuta Kuta
U- Funguo Funguo
U-Kucha kucha
U-Kope kope
v. Ni nomino ambazo zina umbo dhahiri la wingi lakini umbo la umoja halipo
Mfano: Umoja Wingi
Boga Ma-boga
Jembe ma-jembe
Debe Ma-debe
Tako Ma-tako
Panga Ma-panga
iv. Ni majina yanayokuwa na mofimu ya wingi wala umoja
Mfano: Umoja Wingi
Boga ma – maboga
Debe ma - debe
Tako Ma-tako
Panga Ma-panga
v. Ni majina yanayokuwa na mofimu ya wingi wala umoja
Mfano: Umoja Wingi
Shule Shule
Ng’ombe Ng’ombe
Mbuzi Mbuzi
Kuku Kuku
N.B: Mofimu kapa hujitokeza katika kundi la pili (2) na kundi la tatu (3) ambapo katika kundi la pili (2) katika umoja majina yana mofimu (2). Mofimu ya kwanza inaonesha umoja na mofu ya pili inaonesha mzizi wa neno.
Katika wingi mofu ya wingi ni kapa ambayo hufuatiwa na mofu ya pili inaonesha mzazi wa neno. Katika wingi mofu ya wingi ni kopa ambayo hufuatiwa na mofu mzizi na kuzifanya nomino hizo kuwa na mofu mbili. Mofu ya kwanza ni kapa ambayo hudokeza wingi na mofimu ya pili ni mzizi. Japokuwa mofu ya wingi ni kapa yaani haiandikwi wala kutamkwa athari yake ipo.
DHIMA ZA MOFIMU
1.Kuonesha udogo wa kitu au ukubwa wa kitu
Mfano: Kijiti-jiti
Kuondoa upatanisho wa kisarufi ambao hutawaliwa na nomino ya kiima na kitenzi.
Mfano: Kiti kimevunjika.
Utaratibu huu haufai.
Sheria hii haifai.
Kudokeza nafsi mbalimbali.
Mfano: ni....na....som....a-nafsi ya kwanza umoja.
Tu....na....som....a-nafsi ya pili umoja
U-na-som-a- nafsi ya pili wingi
A-na-som-a- nafsi ya tatu umoja
wa-na-som-a- nafsi ya tatu wingi.
4. Kudokea njeo/wakati
Mfano: Atakuja- Wakati ujao
Atakapokuja- Wakati uliopo timilifu.
Amekuja- Wakati uliopita timilifu.
Alikuja- Wakati uliopita.
5.Kudokeza hali mbalimbali katika tungo.
Mfano: Hucheza- Hali ya mazoea.
Akija- Hali ya masharti.
Angekuja
6.Kudokeza urejeshi kwa mtenda mtendwa mtendwa kujitenda au tendo kwa mtenda.
Mfano: Aliyenipiga- Inaturejesha kwa mtenda.
Aliyenipiga- Inaturejesha kwa mtenda.
Aliyesomea-Inaturejesha kwa mtendewa
Nimejikata- Inarejesha tendo kwa mtenda (kujitenda)
7.Kuonesha ukanushi.
Mfano: Hakuja
Sisomi
8. Mofimu hudokeza kauli mbalimbali
Mfano: Kauli ya kutendwa- Pigw-pig-w-a
Kauli ya kutendewa-pig-iw-a
Kauli ya kutendea-pig-i-a
Kauli ya kutenda-pig-a
Kauli ya kutendeana-pig-an-a
Kauli ya kutendeshwa-pig-ian-a
Kauli ya kufungamanisha-gandamana
Kauli ya kutendwa-choma-chomoa
-funga-fungua
Kauli ya kutendaka-fumba- fumbata
-ambaa-ambata
4. Kuonesha udogo wa kitu au ukubwa wa kitu
Mfano: Kijiti – jiti
Kuondoa upatanisho wa kisarufi ambao hutawaliwa na nomino ya kiima na kitenzi
Mfano: Kiti kimevunjika.
Utaratibu huu haufai.
Sheria hii haifai.
Kudokeza nafsi mbalimbali
Mfano: ni ......na.... som ....a – nafsi ya kwanza umoja
Tu... na...som...a-------------nafsi ya pili umoja
U-na-som-a -------------- nafsi ya pili wingi
A-na-so-a------------------- nafsi ya tatu umoja
wa – na—som—a-----------nafsi ya tatu wingi
Kudokeza njeo/wakati
Mfano: Atakuja – Wakati ujao
Atakapokuja – Wakati uliopo timilifu
Amekuja - Wakati uliopita timilifu
Alikuja - wakati uliopita
8. Kudokeza hali mbalimbali katika tungo
Mfano: Hucheza – hali ya mazoea
Akija – Hali ya masharti
Angekuja
9. Kudokeza urejeshi kwa mtenda mtendwa mtendwa jujitenda au tendo kwa mtenda
Mfano: Aliyenipiga – Inaturejesha kwa mtenda
Aliyenipiga – Inaturejesha kwa mtendwa
Aliyesomea - inaturejesha kwa mtendewa
Nimejikata – inarejesha tendo kwa mtenda (kujitenda)
10. Kuonesha ukanushi
Mfano: Hakuja
Sisomi
11. Mofimu hudokeza kauli mbalimbali
Mfano: Kauli ya kutendwa – Pigwa - Pig- w-a
Kauli ya kutendewa pig-iw –a
Kauli ya kutendea- pig –i – a
Kauli ya kutenda –Pig –a
Kauli ya kutendeana – Pig – an –a
Kauli ya kutendeshwa – pig-ian –a
Kauli ya kufungamanisha - gandamana
Kauli ya kutendwa - choma - chomoa
-Funga - fungua
Kauli ya kutendaka - fumba - fumbata
Ambaa – ambata
ALOMOFU
Alomofu ni maumbo zaidi ya moja au maumbo tofauti ambayo huwakilisha mofimu moja kisanji ambayo hufanya kazi moja kisaruji alomaju hutokea mazingira maalum baadhi ya mazingira hutabirika mengine hayatabiriki kabisa. Alomofina kwa kawaida kubadili maana ya neno.
UTOKEAJI WA ALOMOFU
Mazingira ya kifonolojia (matamshi)
Kwa kutumia utawala au mazingira tunaweza kupata mofimu na alama yake kwa vitenzi vya lugha ya Kiswahili vinaponyumbuliwa huzalisha kauli mbalimbali, kauli hizo hudhihirika kutokana na kuwepo kwa mofimu mahususi zinazoonesha kauli husika.
Kauli ya kutendewa
Kauli hii inahusisha tendo ambalo hutendwa na muhusika Fulani kwa niaba ya wahusika mwingine. Maumbo ambayo huonesha kauli hiyo ya kutendwa ni (-iw-) (-ew-) na (-liw-) na (-lew-). Mambo haya hufahamika kama alomofu na utokeaji wake hutegemea athari za kimatamshi za kitenzi husika
Mfano: Lima - Lim – iw –a
Suka - suk – iw – a
Cheza – chez – ew –a
Paka - pak – iw – a
Soma – som – ew –a
Kimbia – kimb – liw –a
Tafiti – tafit – iw –a
Zoa – zo – l-ew –a
Chomoa – chomo – lew –a
Mofimu ya kauli ya kutendewa ina alomofu tano ambazo ni
(-iw-) hii hutokea ikiwa mzizi wa kitenzi unaishia na konsonanti na mzizi huo una irabu a,e,I,o,u.
(ew-) hii hutokea ikiwa mzizi wa kitenzi unaishia na konsonanti na mzizi huo unairabu e au o
(-liw-) hutokea ikiwa mzizi wakitenzi unaishia na irabu i, a , au u
(-lew-) hutokea ikiwa mzizi wa kitenzi unaishia na irabu a au e
(-w-) hutokea kama mzizi wa kitenzi unaishia na irabu- i -lakini kwa vitenzi vya kuchukua yaani visivyokuwa na asili ya kibantu.
Mazingira ya kileksika
Kwa kutumia mazingira ya kileksika alomofu zinaweza kutokea katika ngeli za majina kwa mfano katika ngeli ya kwanza na y apili yaani m/w inaweza kuona alomofu ageli ya kwanzakama ifuatavyo:-
NGELI II NGELI 1
Wa –tu M-tu
Wa-ke M-ke
Wa-nafunzi Mw-anafunzi
Wa-elevu Mw-elevu
Wa-wezeshaji Mw-ezeshaji
Wa-imbaji Mw-imbaji
Wa-ongozaji Mw-ongozaji
Wa-uguzi Mu-uguzi
Wa-umbaji Mu-mbaji
Katika ngeli ya kwanza mofimu m –inaonesha umoja .katika ngeli hiyo ya kwanza ambayo kiwakilishi chake ni mofimu m- kuna maumbo matatu ambayo hufanya kazi ya kuonesha umoja katika ngeli- I- maumbo hayo ni;
Kwa hiyo ngeli ya I ina alomofu tatu alomofu ni (m-) (mw-) (-mu-)
Alomofu (m-) hutokea inapofuatwa na konsonanti
Alomofu (m-) hutokea inapofuata na irabi a, e, i, o
Alomofu, (mu-) hutokea inapofuatwa na irabu- w
Mazingira ya kisarufi
Kwa kutumia mazingira ya kisarufi tunaweza kupata mofimu na alomofu zake hasa katika mofimu njeo. Mofimu rejea inawakilishwa na maumbo yafuatayo.
a-li – soma
a-me – soma
a-na-soma
a- Ta- soma
Mofimu njeo inaolomofu nne alomofu hizo ni (-li-) (-me-) (-na-) na (-ta-)
Alomofu (-li-) na (-ta-)
Alomofu (-me-) hutokea kuonesha wakati uliopita timilifu
Alomofu (-na-) hutokea kuonesha wakati uliopo
Alomofu (-ta-) hutokea kuonesha wakati ujao.
N.B: ingwa alomofu ni maumbo yanayotofautiana hufanya kazi moja kisarufi. Maumbo hayo hutokea katika mazingira maalumu ambayo yanaweza yakatabirika au yasitabirike kabisa mazingira hayo yanaweza kuwa ya kifonolojia au mazingira ya kileksika na mazingira ya kisarufi.