Skip to main content




NOMINO /MAJINA (N)
Majina ni aina ya maneno ambayo hutaja vitu, viumbe, hali au matendo ili kuviainisha na kuvitofautisha na vitu vingine.
Mfano: Winnie, Werevu, Wema, Lulu, Mtu, Ubungo, Mungu na n.k
AINA ZA MAJINA
a.Majina ya kawaida
Majina haya yanataja viumbe kama vile wanyama, miti, watu, ndege, wadudu.
Majina yote hayo yanapoandikwa huanza kwa herufi ndogo kama yanatokea katikati ya sentensi au tungo.
N:B Majina hayo sio maalumu kwa vitu Fulani tu bali kwa vitu mbalimbali.
b. Majina ya Pekee.
Haya ni majina maalumu kwa watu au mahali ambaye huonesha upekee kwa watu,mahali au vitu, Majina haya hujumuisha majina binafsi ya watu na majina ya mahali.
Mfano: Marcus, Halima, James, Abel, Fredy, Anna Ubungo, Manzese, Tanzania, Uingereza, Africa
N: B Majina hayo yanapoandikwa huanza kwa herufi kubwa
C. Majina ya jamii.
Haya ni majina ambayo yanataja vitu au watu wakiwa katika makundi au mafungu japo huwa majina hayo yapo katika hali ya umoja. Mfano, Chama , kamati, kadamnasi, timu
d. Majina dhahania
Haya ni majina yanayotaja dhana zinazofikirika zisizonekana kwa macho wala kushika
Mfano:Afya, utajiri, upole ukatili, Mungu, shetani, malaika, Majina yote hao yanapandikwa yapo ambayo huanzia herufi kubwa hata kama huandikwa katikati ya sentensi


e. Majina ya wingi
Haya ni majina ambayo yanadokeza dhana ya wingi japokuwa majina haya hayana umoja wala umbo la majina haya hufanana na majina yaliyopo kwa wingi ingawa mfanano huo hauwiani moja kwa moja na majina ya wingi, Majina hayo umoja na wingi wake hudhihirika kutokana na upatanishi kisarufi uliopo baina ya majina hayo na vitendo
Mfano: wa majina hayo ni kama vile maziwa,mazungumzo, marashi, maji, mafuta manukato, madhehebu.


N:B Majina haya huwa hayana umoja wala wingi japokuwa baadhi ya wazungumzaji huwa wanalazimisha. Dhana ya wingi huwa inadhihirishwa na upatanishi wa kisarufi


Mfano: Maziwa yameharibika
Maziwa mengi yameharibika
Mafuta yamemwagika
Mafuta mengi yamemwagika


II. KIWAKILISHI (W) Kibadala /vijina)
Huwa ni maneno ambayo hutumika badala ya jina au ni maneno ambayo huwakilisha jina. Aina hii ya maneno huwa haitokei kama majina yametumika bali hutokea endapo tu majina hayapo.
N:B Viwakilishi haviwezi kutokea pamoja na majina katika sentensi
∙ Mfano: wewe ni mzuri
W

∙ Wao wanaogopa matokeo
W

∙ Wangapi watafaulu mtihani
W


∙ Huyu aliyekuja amefaulu mtihani
W
AINA ZA VIWAKILISHI
Kuna aina kuu tano za viwakilishi katika lugha ya Kiswahili, ingawa baadhi ya wanasarufi huainisha viwakilishi zaidi ya hivyo,
a. Viwakilishi vya nafsi
Hivi ni viwakilishi ambavyo hutaja nafsi au huwa kilisha nafsi mbalimbali.


Mfano;
∙ Mimi ninasoma (nafsi ya kwanza umoja)
W
∙ Sisi tunasoma (nafsi ya I wingi)
W
∙ Wewe unasoma (nafsi ya II umoja)
W
∙ Yeye anasoma (nafsi ya III umoja)
W


∙ Wao wanasoma (nafsi ya III wingi)
W
b. Viwakilishi vya Mahala/ vioneshi
Hivi ni viwakilishi ambavyo huonyesha kitu kilipo
Mfano: Hawa ni wafanyakazi wa St. Mery Goreti
W
Huyu ni mlevi sana
W
Yule ni mtoto
W
C. Viwakilishi viulizi
Hivi ni viwakilishi ambavyo hutumika kuuliza swali ambalo hurejelea kwenye nomino husika
∙ Mfano: Lipi linakuchanganya
W
Wangapi wamefaulu?
W
d.Viwakilishi vimilikishi
Hivi ni viwakilishi ambavyo huonesha umiliki ambao huvumishwa moja kwa moja na nomino inayohusika
Mfano: Kwetu pazuri
W
Wangu ninampenda
W
Kwenu ni pazuri
W
e. Viwakilishi vya kurejesha
Hivi ni viwakilishi ambavyo hurejesha tendo kwa mtenda au mtendwa na mara nyingi huundwa na mzizi wa amba – pamoja na viambishi vya urejeshi
Mfano: Ambao wamechelewa wameadhibiwa
W
Ambazo zimejengwa barabarani zibomolewe
W
Ambavyo vimeharibika vitupwe
W
Aliyepotea amepatikana
W
III VIVUMISHI (V)
Vivumishi ni maneno au kikundi cha maneno ambacho hutoa maelezo zaidi kuhusu nomino au kiwakilishi. Vivumishi ni maneno yanayovumisha majina au viwakilishi vilivyomo katika tungo. Maelezo hayo ambayo huumbwa na majina yanaweza kuwa na tabia ya jina au idadi ya jina n.k
AINA ZA VIVUMISHI
Wataalamu wa sarufi ya Kiswahili wanatofautiana na katika uainishaji wa aina za vivumishi lakini pamoja na kutofautiana huko wanaonekana kukubaliana katika aina kuu nane (8) za vivumishi
a. Vivumishi vya idadi
Hivi ni vivumishi ambavyo huonesha idadi ya vitu watu au majina mengine yaliyotajwa. Vivumishi hivi huweza kutaja idadi ya vitu waziwazi lakini wakati mwingine hutaja idadi ya vitu katika orodha,
Mfano: Mikate mitano
V
Watu wengi
V
Ghorofa ya kumi
V
Chai kidogo
V
Maji mengi
V
b. Vivumishi vya sifa
Hivi ni vivumishi vinayosifia majina wakilishi vilivyopo katika tungo
Mfano: Mkulima hodari
V
Msichana mrembo
V
Nchi masikini
V
Uchumi dhaifu
V
c. Vivumishi vya kumiliki
Hivi ni vivumishi ambavyo huonesha umiliki wa kitu watu au wanyama
Mfano: Kitabu changu
V
Shule yake
V

Vivumishi vioneshi
Hivi ni vivumishi vinavyoonesha mahali kitu kilipo au mtu alipo huitwa vivumishi vya mahali kwa sababu vinaonesha mahali.
Mfano: Mtoto huyo.
V

Mtoto huyo
V
Mtoto yule
V

Vivumishi viulizi
Hivi ni vivumishi amabavyo huuliza ili kupata idadi ya watu au vitu.
Mfano: Vitabu vingapi vimenunuliwa?
V

Kiongozi gani amekuja?
V

Vivumishi vya jina kwa jina
Hivi ni vivumishi amabavyo huwa ni majina yanayovumisha au kutoa maelezo zaidi kuhusu majina mengine.
Mfano: Mtoto kiziwi
V

Mpenzi jini
V

Mpenzi bubu
V

Mzee bubu
V
Vivumishi vya a-unganifu.
Hivi ni vivumishi ambavyo huwa na jina lenye-a-ya uunganifu.
Mfano: Mambo ya kihuni
V

Chakula cha watoto.
V

Nguo za kichina
V

Vivumishi vya pekee.
Hivi ni vivumishi ambavyo huonesha ziada ya kitu, mtu au jina lolote lililotajwa.
Mfano: Mtu mwenyewe haeleweki
V
Sisi sote ni ndugu
V
Ninyi nyote ni wanafunzi
V


VITENZI
Kitenzi ni neno ambalo hutaja jambo lilitendwa, linalotendwa au litakalotendwa na kitu, mtu au kiumbe chochote kile chenye uwezo wa kutenda tendo husika. Aidha kitenzi huonesha tabia au hali inayoweza kuwepo au kutokuwepo kwa mtu, kitu au kiumbe kingine chochote kile.

NB; Katika lugha ya kiswahili vitenzi huwa havitumiki pekeake bali huambatana na viambishi ambavyo hudokeza nafsi ya mtendwa au mtenda, wakati tendo lilipofanyika pamoja na kauli ya tendo.
mfano:
Kula - Anakula


Vivumishi vioneshi
c. Hivi ni vivumishi vinavyoonesha mahali, kitu kilipo au mtu alipo huitwa vivumishi vya mahali kwa sababu vinaonesha mahali.
∙ Mfano: Mtoto huyo
V
∙ Mtoto huyo
V
∙ Mtoto Yule
V
∙ Yule mtoto amepotea
V
e. Vivumishi viulizi
Hivi ni vivumish ambavyo huuliza ili kupata idadi ya watu au vitu
Mfano: Vitabu vingapi vimenununuliwa?
V
Kiongozi gani amekuja?
V
f. Vivumishi vya jina kwa jina
Hivi ni vivumishi ambavyo huwa ni majina yanayovumisha au kutoa maelezo zaidi kubuni majina mengine
Mfano: Mtoto kiziwi
V
Mpenzi jini
V
Mpenzi Bubu
V
Mzee bubu
V
g. Vivumishi vya a- Unganifu
Hivi ni vivumishi ambavyo huwa na jina lenye- a – ya uunganifu
Mfano: Mambo ya kihuni
V
Chakula cha watoto
V
Nguzo za kichina


h. Vivumishi vya pekee
Hivi ni vivumishi ambavyo huonesha ziada ya kitu, mtu au jina lolote lililotajwa
Mfano: Mtu mwenyewe haeleweki
V
Sisi sote ni ndugu
V
Ninyi nyote ni wanafunzi
V
IV. VITENZI
Kitenzi ni neno ambalo hutaja jambo lililotendwa, linalotendewa, au litakalotendwa na kitu, mtu au kiumbe chochote kile chenye uwezo wa kutenda tendo husika. Aidha kitenzi huonyesha tabia au hali inayoweza kuwepo au kutokuwepo kwa mtu, kitu au kiumbe kingine chochote kile.
N.B: Katika lugha ya Kiswahili vitenzi huwa havitumiki peke yake bali huambatana na viambishi ambavyo hudokeza nafsi ya mtendwa au mtenda, wakati tendo lilipofanyika pamoja na kauli ya tendo.
Mfano:
Lala - Anaimba
Kula - Anakula
AINA ZA VITENZI
Wataalamu wa lugha ya Kiswahili wanatofautiana katika uanishaji wa aina za vitenzi, wapo wanaoainisha aina kuu tatu (3) yaani kitenzi kikuu (T) kitenzi kisaidizi (Ts) na kitenzi kishirikishi (t). na wapo wanaoainisha aina kuu (2) yaani kitenzi halisi na kitenzi kishirikishi
N.B Katika uainishaji wa vitenzi, tutashughulikia uainishaji wa aina kuu mbili (2) za vitenzi yaani vitenzi halisi na vitenzi vishirikishi.
a. Kitenzi halisi
Hivi ni vitenzi ambavyo hueleza matendo. Katika lugha ya Kiswahili kitenzi halisi kinaweza kutumika kimoja au zaidi ya kimoja katika sentensi. Vitenzi vinapotumika humbatana na viambishi ambavyo hudokeza nafsi wakati halisi au kauli ya tendo na hivyo kwa pamoja hufanya kifungu tenzi halisi.
Aina za vitenzi halisi
Kuna aina kuu mbili (2) za vifungu tenzi halisi
- Kifungu tenzi halisi kikuu (T)
- Kifungu tenzi halisi kisaidizi (TS)
1. kifungu tenzi halisi kikuu (T)
Hiki ni kifungu tenzi ambacho hueleza tendo lililofanywa, litakalofanywa au linalofanywa na mtendo au tendo alilofanyiwa, analofanyiwa au atakalofanyiwa mtendwa kutokana na sifa hii vitenzi hubeba nafsi ya mtenda, mtendwa wakati tendo lilipofanya pamoja. hali kauli ya tendo sifa hizi huzifanya kitenzi kuwa aina ya neno inayobebeshwa mzigo mkubwa katika lugha ya Kiswahili.
∙ Mfano: Juma alikula chakula
T
∙ Juma anakula chakula
T
∙ Juma atakula chakula
T


II. KIFUNGU TENZI HALISI KISAIDIZI (TS)
Hiki ni kitenzi ambacho huambatana na kitenzi halisi kikuu na aghalabu huoneshwa wakati tendo lilipofanyika na pia hudokeza uyakinishi au ukanushi wa tendo. Kifungu tenzi halisi kisaidizi hutumika sambamba na kifungu tenzi halisi kikuu.
Kikitumika peke yake bila kuambatana na kitenzi kikuu basi dhima yake hubadilika na kuwa kitenzi kikuu kikiondolewa katika tungo, Kitenzi kisaidizi huchukua dhima ya kitenzi kikuu.
Mfano: Juma anataka kula chakula
Ts T
Juma anataka chakula
T


N.B: Katika sentensi ya pili kitenzi anataka kimechukua dhima ya kitenzi kikuu baada ya kuondoa kitenzi kile ambacho kilikuwa kitenzi kikuu katika sentensi ya kwanza. Pia vitenzi visaidizi vinaweza kutumika zaidi ya kimoja katika sentensi visaidizi vinaweza kutumika zaidi ya kimoja katika sentensi.


∙ Mfano: Juma alikuwa anataka kwenda kusoma
TS TS T

b. Kitenzi kishirikishi (t)
Haya ni maneno yanayoonyesha tabia au hali Fulani iliyopo kwa mtu au kitu Fulani vitenzi vishirikishi ambavyo huonesha tabia au hali Fulani iliyopo kwa mtu au kitu huitwa vitenzi vishirikishi yakinishi. Na vitenzi vishirikishi ambavyo huonesha kutokuwepo kwa hali au tabia kwa mtu au kitu huitwa vitenzi vishirikishi vikanushi.
N:B Mara nyingi katika lugha ya Kiswahili kitenzi kishirikishi yakinishi ni “ni” na kitenzi kishirikishi ni na kitenzi kishirikishi kanushi “si” Lakini kuna vitenzi vingine vishirikishi zaidi ya hivyo katika lugha ya Kiswahili
Mfano
∙ Juma ni mtoto
t
∙ Juma si mtoto
t
∙ Juma siyo mwizi
t
∙ Udongo u mkavu
t
∙ Babu yu mkali
t
∙ Kitabu ki kidogo
t
∙ Mchungwa u mkubwa
t
∙ Midomo i minene
t
∙ Ubao u mpana
t
∙ Mbao zi pana
t
∙ Hapa pa pachafu
t
∙ Huku ku kuzuri
t
∙ Humu mu mweusi
t
∙ Chakula ndicho kitamu
t
∙ Anna ndiye mgonjwa
t
∙ Juma angali mtoto
t
∙ Wanafunzi hawa wangapi wadogo
t
Maneno yote yaliyopigiwa mstari ni vitenzi vishirikishi


KAULI ZA VITENZI
Vitenzi vya lugha ya Kiswahili vinatabia ya kunyumbuka na hivyo kuzalisha kauli mbalimbali za vitenzi. Kauli hizo ni kama zifuatazo
Mfano:


ii. Kauli ya kutendwa
Mfano: Pigwa
Somwa
Limwa
Chezwa


iii. Kauli ya kutendeka
Mfano: Pigika
Valika
Someka
Limika




iv. Kauli ya kutendana
Mfano: Pigana
Vaana
Toana
Somana

v. Kauli ya kutendana
Mfano: Iimiana
Someana
Valiana
Toleana




vi. Kauli ya kutendechwa
Mfano: Shoneshwa
Someshwa
Limishwa
Valishwa


vii. Kauli ya kutendea
Mfano: Pigia
Somea
Limia
Zalia


viii. Kauli ya kutendwa
Mfano: Pigiwa
Somewa
Shonewa
Chezewe


HALI ZA TENDO
Vitenzi vya lugha ya Kiswahili vinavyotumika huweza kuonesha hali tofauti kutokana na kuambishwa viambishi tofauti. Baadhi ya hali katika vitenda hujitokeza zaidi katika mazungumzo na nyingine mara chache
i. Hali ya masharti
Hali hii huonesha kuwa kufanyika kwa tendo Fulani sharti kutanguliwe na tendo lingine. Lazima kuwa na matendo mawili yaliyofuatana.
Mfano: Wangecheza kwa umakini wangepata ushindi
Akija nitamwambia
ii. Hali ya kuendelea kwa tendo
Hali hii huonekana katika tendo ambalo linaendelea kufanyika hili huziirishwa na mofu ya wakati “na” ambayo hupachikwa katika vitenzi.
Mfano: Anasoma
Anakula
N: B Pia hali ya kuendelea kwa tendo inaweza ikadokezwa na kiambishi “ki” ambacho aghalabu hutokea katika kitenzi cha pili katika sentensi yenye vitenzi sambamba.
Mfano: Aliniona nikisoma
N.B: Pia hali ya kuendelea kwa tena hudokezwa na kiambishi “Ka” katika masimilizi ya matendo yoliyofululizana katika masimulizi ya matukio mbali mbali, yaliyofanyika moja baada ya jingine kimsingi yalipaswa kutumia kiambishi “li”ambacho hudokeza wakati uliopita lakini matumizi yake humchosha msemaji na msikilizaji lakini pia ni kwa kurudia rudia na kurejesha sentensi bila sababu hivyo kiambishi “ka” hutumika badala ya “li”


Mfano: Tulifika chuoni tukapokelewa na mkuu wa chuo, akatupa funguo za bweni akatuonesha pakulala na katupa magodoro na mablanketi akatupeleka kafteria. Akatugawia sahani vijiko na visu akaagiza tugewe chakula kisha tukaenda kulala


iii. Hali ya mazoea
Hii ni hali inayoonesha kujirudia rudia kwa tendo au mazoea ya kufanya tendo Fulani
Mfano: Baba huamka asubuhi na mapema
Juma hucheza mpira wa miguu
N.B: Hali ya mazoea hudokezwa na kiambishi "hu"


iv. Hali timilifu
Hali timilifu katika vitenzi huonyesha kukamilika kwa tendo yaani tendo limekwisha kufanyika lakini athari za tendo hilo bado zinaonekana, kiambishi kinachotakiwa cha hali timilifu ni “me” katika hali ya uyakinishi katika hali ya ukanushi ni "ja"


Mfano:
∙ Juma amekimbia
∙ Juma hajakimbia
∙ Wazazi wake wamehama Tanga
∙ Mama hajapika chakula


v. Hali ya kuamuru (amri)
Hii ni hali ambayo hujitokeza katika kifungu tenzi na kawaida hudokezwa katika vitenzi na kiambish tamati “a” katika umoja nakiambashi tamati “eni” katika wingi paispo kumbatana na viambishi vya wakati.
Mfano: Umoja Wingi
Soma Som – oni
Tokea Tok – eni


vi. Hali ya kuhimiza
Hii ni hali ambayo hujitokeza kwenye vifungu tenzi kwa lengo la kusihi, au kumuomba mtu afanye jambo Fulani au asifanye jambo Fulani. Hali ya kutimiza hudokezwa na kiambishi “e” ambacho huwekwa mwishoni mwa kitenzi kwenye vitenzi vinayohusu nafsi ya kwanza umoja kwa vitenzi vinayohusu nafsi ya kwanza wingi hali ya kuhimiza huoneshwa na kiambish tamati “eni” ambacho huwekwa mwanzoni mwa kitenzi.
Mfano
Nilal-e
Niend –e
Tuend-eni


vii. Hali ya kutarajia
Hali huonesha matarajio ya kutendeka kwa jambo pasipo kuwa na uhakika wa kutimia kwa nia hiyo
Mfano:
Nipende
Tupendane


N.B: Hali ya kutarajia pia hudokezwa na kiambishi tamati “e”
ALAMA ZA WAKATI KATIKA KITENZI
Maranyingi vitenzi katika lugha ya Kiswahili huambatana na viambishi mbalimbali ambavyo hudokeza dhana mbalimbali na hivyo kufanya kazi kama kifungu tenzi. Kwa ujumla lugha ya Kiswahili ina nyakati kuu tatu zinazotumika zaidi yaani wakati uliopita wakati uliopo na wakati ujao. Nyakati hizi hudokezwa na viambishi mahususi vya matendo yanapokuwa katika yakinifu na yanapo kanushwa.
∙ WAKATI ULIOPITA
Wakati uliopita katika lugha ya Kiswahili hudokezwa na viambishi “–li” vitenzi vinapokuwa katika uyakinishi na kiambishi –ku- vitenzi hukanusha. Viambishi hivyo hutanguliwa na viambishi vingine kama vile viambishi vya nafsi na vya ukanushi.
Mfano:
Ni-li-kula si-ku-la
Tu-li-kula ha- tu- kula
U-li-kula hu-kula
M-li-kula ha-m-kula
A-li-kula ha-kula
Wa-li-kula ha-wa-kula
Ni-li-soma si-ku-soma
Tu-li-soma ha-tu-ku-soma
U-li-soma hu-ku-soma
M-li-soma ha-m-ku-soma
A-li-soma ha-ku-soma
Walisoma ha-wa-ku-soma


N:B Hata hivyo vitenzi vya mzizi wa silabi moja huwa wakati uliopita vitenzi hivyo vinakuwa katika ukanushi kwa sababu ya athari za kimatamshi
∙ WAKATI ULIOPO
Wakati uliopita huonesha tendo linaloendelea kufanyika na kiambishi kinachodokeza wakati uliopo ni –na-“vitenzi vinapokuwa katika ukanushi kiambishi –i- hupachikwa mwishoni mwa vitenzi.
Mfano:
Ni-na-kula si-l-i
Tu-na-kula ha-tu-l-i
U-na-kula hu-l-i
M-na-kula ha-m-l-i
A-na-kula ha-l-i
Wa-na-kula ha-wa-l-i


∙ WAKATI ULIOPO TIMILIFU
Wakati timilifu katika lugha ya Kiswahili hudokezwa na mofimu –me- vitenzi vinapokuwa ktika uyakinishi na mofimu –ja- vitenzi vinapokuwa katika ukanushi
Mfano: ni-me-soma si-ja-soma
Tu-me-soma hu-tu-ja-soma
U-me-soma hu-ja-soma
A-me-soma ha-ja-soma
Wa-me-soma ha-wa-ja-soma
V. VIELEZI (E)
Vielezi ni aina ya maneno ambavyo hutoa maelezo zaidi kuhusu kitenzi, kielezi mara nyingi hujibu maswali kama tendo limefanywa mara ngapi ? tendo limefanywa namna gani ? tendo limefanywa lini ? na wapi ?
AINA YA VIELEZI
Vielezo vipo vya aina kuu tano
a. Vielezi vya namna /jinsi
Hivi ni vielezi ambavyo huonesha namna ambavyo tendo lililofanywa, linavyofanywa au litakavyofanywa
Mfano; Wanafunzi wanasoma kwa bidii
Mwizi alipigwa sana
Nilimuona kwa macho yangu
b. Vielezi vya idadi/kiasi
Hivi ni vielezi ambavyo hueleza kiasi ambacho tendo limefanyika, mfano tendo limefanyika mara nyingi au mara chache
Mfano: Debe limejaa pomoni
E
Alianguka chini mara tatu
E
Anaenda shuleni mara chache sana
E
c. Vielezi vya mahali/vioneshi
Hivi ni vielezi ambayo hueleza mahali ambapo tendo limefanyika
Mfano: Tuliambiwa twende darasani
E
Juma anaishi Arusha
F
Mwalimu amekwenda nyumbani
E
d. Vielezi vya wakati
Hivi vielezi ambavyo hudokeza muda au wakati tendo lilipofanyika
Mfano: Mvua imenyesha usiku kucha
E
Njoo kesho asubuhi
E
Tutafanya mtihani Alhamisi
E
e. Vielezi viingizi
Hivi ni vielezi ambavyo hueleza tendo lilivyofanyika kwa kuigiza au kufuatisha mlio wa sauti unaajitokeza wakati tendo husika inapotendeka
Mfano: Mbwa alilia bwe
E
Alidondoka chini puu
E


N: B Jambo la msingi la kuzingatia katika vielezi ni kwamba kielezi uhusiana na kitenzi, kielezi hutokea baada ya kitenzi au baada ya shamirisho na wakati mwingine kielezi kinaweza kutanguliwa kabla ya kitenzi.
Mfano: Juma anacheza mpira uwanjani
Sh E
Juma anacheza uwanjani
E
Aliponiona alikimbia
E
VI. VIIGIZI/VIINGIZI/VIHISISHI (J)
Haya ni maneno yanayodokeza vionjo au miguso ya moyoni au akilini aliyokuwa nayo mzungumzaji. Viingizi hudokeza hisia kama vile za furaha, huzuni, uchungu, kushangaa, kushtuka, laana, matumaini au kukata tamaaa, huruma na n.k


Mfano: Ebo! unaumwa nini?
I
Yanga zii!
I
Lah! Naipenda kweli
I
Mmh! We hujui tu
I
N.B: vihisishi mara nyingi vinapotumika katika maandishi huambatana na alama ya mshangao
VII. VIUNGANISHI (U)
Ni maneno au kikundi cha maneno, chenye kuunganisha kirai, kishazi au sentensi.
Dhima kubwa ya viunganishi ni kuunganisha vipashio viwili au zaidi vyenye hadhi sawa kisarufi. Mfano: Jina na jina kishazi na kishazi, kitenzi na kitenzi, sentensi na sentesi
Mfano; Shangazi na mjomba wanapendana sana
U
Aje Juma au Hamisi
n U


Vitabu vyote vya mama yangu
U


AINA ZA VIUNGANISHI
Viunganishi vinaweza vikagawanywa katika makundi makuu mawili
a. Viunganishi huru
Hivi ni viunganishi ambavyo husimama peke yake katika tungo au vipashio vinavyounganishwa.
Kiungo huru kinaweza kutoka katikati ya tungo mbili zinazoziunganisha au mwishoni mwa tungo mbli zinazoziunganishwa


Mfano: Nitukane tu lakini nakupenda
U
Hata ukinitukana nakupenda
U
AINA ZA VIUNGAISHI HURU
Viunganishi huru vinaweza vikagawanywa katika makundi madogo madogo.
a. Viunganishi huru nyongeza
Hivi ni viunganishi ambavyo huelekeza dhana ya kuongezwa idadi ya vitajwa au matendo yanayosimuliwa


Mfano: Juma na zaina wanaondoka kesho
U
Aliiba chakula kisha akaiba na sahani
U
b. Viunganishi huru chague


Hivi ni viunganishi huru ambavyo hudokezwa maana ya uchambuzi wa vitajwa au matendo
Mfano: Sinywi pombe wala kuvuta sigara
U
Utaondoka leo ama kesho
U


c. Viunganishi huru linganishi


Hivi ni viunganishi ambavyo hudokeza hali ya kulinganisha iliyopo katika tungo mbili au zaidi
Mfano: Nakupenda ingawa hunitaki
U
Juma hakufaulu sembuse Ali afaulu
U
Aliondoka mapema lakini alichelewa kufika
U
d. Viunganishi huru sababu
Hivi ni viunganishi ambavyo hudokeza sababu au matokeo ya matendo yaliyofanyika
Mfano: Alifeli mtihani kwa sababu hakusoma
Ijapokuwa nakupenda usininyanyase
Unaongea kama hutaki
-Iliopigiwa mstari ni viunganishi.
AINA ZA VIUNGANISHI TEGEMEZI
Hivi ni viunganishi ambavyo huwa na kiambishi cha O – ya urejeshi ambayo huwekwa katika kitenzi cha kishazi tegemezi ili kukiunganisha na kitenzi kikuu cha kishazi huru ambavyo kwa pamoja huunda sentensi changamano.
N.B Viambishi tegemezi huwa ni viambishi, lakini wakati mwingine pia huweza kuwa ni maneno maalumu. Pia viunganishi tegemezi vinawezakutokea mwanzoni mwa tungo mbili zinazounganishwa
Mfano: Aliponiona alikimbia
U
Chakula kilichobaki kimechacha
U
Katika sentensi hizo viunganishi tegemezi ni –po- na – cho-, ambapo kiunganishi –po- kinaunganisha chakula kilibaki na chakula kimechacha.
Wakati mwingine pia viunganishi tegemezi huweza kujitokeza kama maneno
Mfano: Ijapokuwa nilimkataza alimpiga
U
Ingawa hakusoma alifaulu
U
VIII VIHUSISHI (H)
Haya ni maneno yanayoonesha uhusiano baina ya tungo mbili zenye maadhi tofauti kisanii
Mfano: Uhusiano kati ya kitenzi na jina
Anatembea kwa miguu
H
Anakula kwa kijiko
H
Simama mbele ya nyumba
H
Huyu ni mtu mwenye maneno mengi
H


N:B: Baadhi ya wanasarufi huchanganya dhana ya viunganishi na vihusishi lakini ukweli ni kwamba dhana ya viunganishi na vihusishi hutofautiana. Tofauti hii hutokana na dhima ya dhana hizo katika tungo. Kwamba dhima ya viunganishi ni kuunganisha tungo zenye hadhi sawa kisarufi wakati dhima ya vihusishi ni kuonesha uhusiano uliopo baina ya tungo mbili zenye hadhi tofauti kisarufi.


AINA ZA VIHUSISHI
a. Vihusishi vya Mahala
Ni vile ambavyo huonesha uhusiano wa Mahala baina ya tungo mbili


Mfano Aliweka katika sanduku
H
Alikaa mbele ya mlango
H
b. Vihusishi vya wakati
Hivi huonesha uhusiano wa wakati baina ya tungo mbili
Mfano: Alifika baada ya masaa machache
H
c. Vihusishi vya sababu
Hivi huonesha sababu au uhusiano uliopo kwa kutokea kwa jambo Fulani baina ya tungo mbili
Mfano: Alipigwa kwa ajili ya makosa yake
H
d. Vihusishi vya ulinganishi
Hivi huonesha uhusiano wa kimlinganisho baina ya tungo mbili
Mfano: Ng’ombe ni mmoja kuliko mbuzi
H
e. Vihusishi vya namna au jinsi
Hivi vinaonesha uhusiano wa kinamna baina ya tungo mbili
Mfano: nataka maji ya moto
H
f. Vihusishi vimilikishi
Hivi honesha uhusiano wa kumiliki baina ya tungo mbili
Mfano: Aliiba fedha za kanisa
H

g. Vihusishi vya ala (chombo kilichohusika)
Hivi huonesha uhusiano uliopo baina ya tendo na kitukilichotumika katika tendo hilo
Mfano: Alipigwa kwa fimbo
H

Maswali
1. Nini tofauti kati ya viwakilisi na majina?
2. Kuna uhusiano gani kati ya nomino na vivumishi au viwakilishi na vivumishi
3. Vitenzi vishirikishi katika lugha ya Kiswahili si vingi lakini ni muhimu jadili
4. Si kila kiambishi huambatana na mzizi kwa namna ile ile jadili kwa mifano
5. Kuna tofauti gani kati ya tungo na sentensi?
6. Kirai ndiyo msingi wa muundo wa tungo nyingine Thibitisha kwa mifano
7. Vivumishi katika lugha ya kiswahihi havina uhai nje ya umbo la kirai nomino thibitisha kwa mifano.


2. KIRAI/KIKUNDI
Kirai ni kipashio au tungo yenye neno moja au zaidi lakini isiyokuwa na muundo wa kiima na kiarifu. Muundo wa kiima na kiarifu ni muundo uoneshe mtenda na jambo linalotendwa au mtendwa wa jambo na jambo analotendwa. Kuna miundo mbalimbali ya kirai ambayo uhusisha neno moja au zaidi ambayo huwekwa kwa pamoja kwa kuzingatia mpango maalumu ambao huzingatia uhusiano baina ya neno kuu na maneno mengine ambayo huambatana na neno kuu.
Mfano: Kirai nomino
Katika kirai nomino neno kuu ni nomino hivyo muundo wake umekitwa kwenye nomino na neno au fungu la maneno.
Mfano: Mtoto yule mwembamba
KN
Miti ile mitatu mirefu
KN

SIFA ZA KIRAI
Kirai kina sifa mbalimbali ambazo hukifanya kirai kiweze kutambulika kiurahisi
i. Kirai hakina kiima na kiarifu muundo ambao huonesha mtenda na jambo analolitenda, tungo nyingine ni neno, kishazi na sentensi


ii Kirai hujengwa na neno moja moja au zaidi ya moja kwa kuzingatia uhusiano uliopo baina ya neno kwa maneno mengine
iii Hutegemea uhusiano maalumu baina ya neno, na maneno mengine yanyohusiana na neno kuu (uainishaji wa virai)
Mfano: Katika kirai nomino neno kuu ni nomino katika kirai kiunganishi neno kuu ni kiunganishi.
iV. Kirai huweza kutokea upande wa kiima au kiarifu katika sentensi
V. Kirai ni tungo kubwa kuliko neno, lakini ndogo kuliko kishazi
AINA ZA VIRAI
Kuna aina kuu tano za virai. Ambazo ni
1. Kirai nomino (KN)
2. Krai kivumishi (KV)
3. Kirai kitenzi (KE)
4. Kirai kielezi (KE)
5. Kirai kiunganishi (KU)


1. KIRAI NOMINO
ni kirai ambacho muundo wake umekitwa kwenye mahusiano ya nomino na maneno mengine na nomino na maneno mengi ambayo yanamahusiano na nomino. Neno kuu katika kirai nomino ni nomino ambayo ndiyo msingi mkuu wa mahusiano na maneno mangine.
MIUNDO YA KIRAI NOMINO
Kirai nomino kina miundo mbalimbali
I.Muundo wa nomino peke yake
Mfano: Cbaki)
Baba
Mama
Winnie
b. II.Nomino mbili au zaidi zilizounganishwa
Mfano: Baba na mama
Baba na bibi
Babu na bibi
Mwalimu na wanafunzi
Mjomba na shangazi
III.Muundo wa nomino na kivumishi kimoja au zaidi
Mfano: Mtoto Mweusi
Watoto wanene wazuri
Watoto na shangazi
IV. Muundo wa nomino na kivumishi kimoja au zaidi
Mfano: Yule mtoto
Watoto wake watatu wanene wazuri
d. V. Muundo wa kivumishi na jina
Mfano: Yule mtoto
Kile kitabu
VI. Nomino na kishazi tegemeza kivumishi
Mfano: Mbwa aliyepata kichaa
f. VII. Nomino , kivumishi na kishazi tegemezi kivumishi
Mfano: Msichana Yule mrembo uliyeniona naye jana
g. VIII.Nomino na kirai kivumishi
Mfano: Mzee mwenye duka kubwa kule kijijini
Watu wengi wenye matatizo ya kifedha
h. IX. Kiwakilishi pekee yake
Mfano: Wewe mimi yeye
i. X. Muundo wa kiwakilishi na kivumishi
Mfano: Vyake vyake
Wao wenyewe
II. KIRAI KIVUMISHI (KV)
Hiki ni kirai ambacho muundo wake umejikita katika kivumishi pamoja na neno au fungu la maneno linaloambatana na kivumishi.
N:B: Ingawa virai vivumishi hujibainisha kimuundo mara nyingi miuundo yake imekuwa ikichukuliwa kama sentensi kwa baadhi ya miundo ya virai nomino
Mfano: Watu wengi wana matatizo ya kifedha
KV
Mfano huu ni wa kirai nomino lakini ndani ya kirai nomino hicho kuna kirai kivumishi ambacho kimepigiwa mstari
MIUNDO YA VIRAI VIVUMISHI
a. Kivumishi na kielezi chake
Mfano: baya sana
Zuri sana
b. Kivumishi na kirai nomino
Mfano: Enye duka kubwa
Enye nguvu nyingi
Enye macho makubwa

c. Kivumishi na kirai kitenzi
Mfano: enye kupenda fujo


d. Kivumish na kirai kitenzi
Mfano: Ingine – enye matatizo


e. Kivumishi na kirai kiunganishi
Mfano: zuri wa kutamanisha
Pungufu wa akili


III. KIRAI KITENZI
Hiki ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusiano na kitenzi au uhusiano baina ya kitenzi na neno au fungu la maneno ambalo huambatana na kitenzi kimahusiano.
MIUNDO YA KIRAI KITENZI
a. Kitenzi peke yake
Mfano: Anaringa
Atapigwa


b. Kitenzi na nomino
Mfano: tumesemewa risala
KT
c. Kitenzi na nomino mbili
Mfano: Tulimpa mtoto chakula
KT
d. Kitenzi na kitenzi
Mfano: Watoto wanaimba wakicheza
KT
e. Kitenzi nomino na kitenzi
Mfano: tulimuomba mwalimu afundishe
KT
f. Muundo wa ruwaza wa kitenzi “kuwa”
Mfano: a. Unaotokana na kitenzi na kivumishi
- Alikuwa mrefu
b. Kitenzi na kirai kiunganishi
- alikuwa na pesa
c. Kitenzi na nomino pahala (kielezi)
- Alikuwa darasani
d. Kitenzi kielezi na kitenzi
-Itakuwa vizuri uwahi
IV. KIRAI KIELEZI (KE)
Tofauti na aina nyingine za virai miundo virai haijakitwa katika mahusiano baina ya neno kuu, yaani kielezi na neno au fungu la maneno linaloandamana na kelezi. Badala yake miundo ya kirai kielezi huwa inahusishwa maneno ambayo hufanya kazi kwa pamoja katika lugha kama misemo tu.
Mfano: Mara kwa mara
-Mara nyingi
-Sana sana
-Haraka haraka
N:B Dhima kubwa ya virai vielezi katika sentensi ni kueleza jinsi, mahali wakati na sababu zilizofanya tendo Fulani lifanyike.
Tofauti na virai vingine ambavyo nafasi yake ndani ya sentensi huwa yakudumu, nafasi ya virai vielezi hubadilika yaweza kuwa mwanzoni au mwishoni mwa sentensi


Mfano: mwalimu alifundisha jana jioni
KE
Jana jioni mwalimu alifundisha
KE
V. KIRAI KIUNGANISHI
Hiki ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusinano baina ya maneno kama vile; kwa, na, katika, na kwenye katika fungu la maneno linaloambatana nacho. Kirai kiunganishini ni kirai ambacho neno kuu ni kiunganishi


NB: Katika lugha ya Kiswahili virai viunganishi vinamuundo mmoja tu nao ni ule wa kiunganishi na kirai nomino
Mfano: Kwa miguu
Kwa amri ya jeshi
Kwa baba yake
Katika chumba
Na mama
Kwenye pombe
Japokuwa virai hivi vinamuundo mmoja, yaani kiunganishi na kirai nomino vinatofautiana sana kimaana.
Mfano: Baadhi ya virai viunganishi vinaonesha dhana ya uhusika naVingine vinadokeza dhana ya mahali au
a. Pahala; - Katika chumba
Kwenye pombe
Kwa baba yake
b.Vingine vinadokeza dhana ya utumishi
Kama vile kwa kijiko
Kwa miguu
C.Vingine hudokeza sababu - kwa amri ya jeshi
3. KISHAZI
Hii ni tungo yenye kitenzi ambacho huweza kujitosheleza na kutoa taarifa iliyokamili au yaweza kuwa na kitenzi kisichojitosheleza na hivyo kushindwa kutoa taarifa iliyokamili au uliokusudiwa na mzungumzaji
Mfano: Msichana uliyemuona jana
Msichana anasoma
Mzee aliyepotea
Mzee amepatikana leo asubuhi
AINA ZA VISHAZI
Kuna aina kuu mbili za vishazi
1. KISHAZI HURU (k/Hr )
Kishazi huru ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kikuu na hivyo kukifanya kishazi hicho kutoa ujumbe unaojitokeza na kisichohitaji maelezo yoyote ya ziada
Mfano: Wanafunzi wanamsikiliza mwalimu
-Mwalimu anafundisha wanafunzi
Vishazi hivi vinajitosheleza kwa sababu vinatoa ujumbe usiohitaji maelezo ya ziada
N:B: Vishazi vinahadhi sawa na sentensi sahili
II KISHAZI TEGEMEZI (K/TG)
Kishazi tegemezi ni kishazi ambacho kinatawaliwa na kitenzi ambacho hakikamilishi ujumbe ulokusudiwa na hivyo kukifanya kutegemea kitenzi kikuu cha kishazi huru ili kukamilisha ujumbe ulikusudiwa na mzungumzaji.
Mfano: -Wanafunzi waliokuwa darasani
- Mwalimu aliyefundisha
Vishazi hivi ni tegemezi kwa sababu vinatoa ujumbe usiojitosheleza hivyo vinahitaji kuandamana na kisha huru ili kukamilisha ujumbe uliokusudiwa.
Mfano : wanafunzi waliokuwa darasani wamefukuzwa shule.
Mwalimu aliyefundisha amesimamishwa kazi.
N:B Kishazi tegemezi hakikamilishi ujumbe mpaka kiandamane na kishazi huru. Kishazi tegemezi kinapoambatana na kishazi huru vyote kwa pamoja hutengeneza sentensi changamano.


AINA ZA VISHAZI TEGEMEZI


Vishazi tegemezi vinaweza kugawanya katika makundi makuu mawili


a. Kishazi tegemezi kivumishi (K/TGV au BV)
b. Kishazi tegemezi kielezi (K/TgE au BE)
KISHAZI TEGEMEZI KIVUMISHI
Vishazi tegemezi vumishi ni vishazi ambavyo huvumisha au hutoa maelezo zaidi kuhusu nomino zilizopo katika tungo, yaani nomino ya kiima au nomino ya shamirisho, kishazi tegemezi, kivumishi kinaweza kutokea kwenye kiima au kiima au kiarifu katika sentensi.
Mfano: Wanafunzi waliotoroka jana wanaadhibiwa leo asubuhi
BV
Mwalimu amewaadhibu wanafunzi waliotoroka jana
BV

KISHAZI TEGEMEZI KIELEZI
Hiki ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi ambacho huwa na utegemezi wa taarifa hiyo huhitaji kukamilisha taarifa hiyo kwa kuambatana na kitenzi kikuu cha kishazi huru. Kishazi tegemezi kielezi hutoa maelezo zaidi kuhusu kitezi kikuu kilichokuwepo katika tungo


Mfano: Alikikata alipolima

BE
Waalimu walipotuma walitufukuza
BE


Sifa za kishazi tegemezi
Kishazi tegemezi kinasifa bainifu ambazo hukifanya kijulikane kiurahisi


i Hakiwezi kutoa maana kamili kama hakijaambatana na kishazi huru
Mfano: Mwalimu alipoanza kufundisha
B
Mzee uliyemuona jana
B
ii. Kinaweza kuondolewa katika sentensi na kisiharibu maana ya sentensi nzima
Mfano: Mbwa aliyepata kichaa ameuwawa
Watoto waliponiona walifurahi
Kinaweza kutambulika kwa kuwepo vishazi vingine kama vile, ingawa, kwamba, ili, kwa sababu, au.
Mfano: -Mwalimu amesema kwamba wanafunzi wengi wamefaulu
- Wanafunzi ambao hawapo wataadhibiwa
B
- Ingawa walifika hatukuwaona
B
- Ili tuweze kuendeleza lazima tufanye kazi Kwa bidii
B
Kinaweza kutanguliwa au kikafuatwa na kishazi huru
Mfano: nimemuona Rehema nilipokwenda
B
HADHI YA VISHAZI
Vishazi huru vinahadhi sawa na sentensi sahili
Mfano: Ng’ombe amechinjwa leo asubuhi
Kishazi tegemezi ambacho huandamana na kishazi huru, hadhi yake hushuka na hivyo kukifanya kuwa na hadhi sawa na kirai /kikundi.
Mfano: Ng’ombe aliyenunuliwa jana
Hiki ni kishazi tegemezi na hadhi yake imeshuka kulingan na kirai tena kira nomino


DHIMA YA VISHAZI
Vishazi vinapotumika katika tungo huwa na dhima mbalimbali


- Vishazi tegemezi vivumishi hufanya kazi kama vivumishi katika tungo.
Mfano: Mtoto asiyesikia amepotea
V
- Baadhi ya vishazi tegemezi hufanya kazi kama vishazi
Mfano: Watoto wanaofurahisha wanavyoimba
E


4. SENTENSI
Sentensi ni kifungu cha maneno kinachoanzia neno moja na kuendelea lakini chenye muundo wa kiima na kiarifu au kikundi nomino na kikundi kitenzi
N.B; Sentensi ndiyo tungo kubwa kuliko tungo nyingine zote katika mpangilio wa tungo


MUUNDO WA SENTENSI
Sentensi ina sehemu kuu mbili (2) Sentensi ikigawanywa kwa kutumia kigezo cha kidhima ina sehemu kuu mbili ambazo ni KIIMA na KIARIFU


Sentensi ikigawanywa kwa kuangalia muundo wa sentensi basi sentensi hugawanywa katika sehemu kuu mbili yaani KIKUNDI NOMINO na KIKUNDI KITENZI.


Mgawanyo huu hutokana na kanuni kuu ya kisintaksia ambayo hudai kila sentensi iliyosahihi na inayokubaliwa na wazawa wa lugha ya Kiswahili ni lazima iwe na muundo wa kiima na kiarifu au kikundi nomino na kikundi kitenzi.
Kiima hutaja mtenda au mtendwa wa jambo na kiarifu huarifu jambo linalotendwa na kiima au alilotendwa na kiima
Mfano: Juma anacheza mpira.
Juma ni kiima yaani mtendwa na kiarifu ni anacheza mpira
Hapa pia nomino mpira ndiyo kiima, lakini kiima hiki kinataja kile kinachotendwa yaani mpira
KIIMA
Kiima ni sehemu ya sentensi ambayo hujaza na nafasi ya mtenda au mtendwa katika sentensi
NB: aghalabu kiima hutokea upande wa kushoto wa kitenzi
Mfano:Mwalimu/anafundisha wanafunzi
K
Wanafunzi/ wanafundishwa na walimu
K
Kwa kawaida kiima hukaliwa na jina au kikundi jina ambalo hujaza nafasi ya mtenda au mtendwa katika sentensi
VIPASHIO VYA KIIMA
Kiima kinajengwa na nini?
Kiima hujengwa na vipashio vifuatavyo
i. Jina peke yake
Mfano: Mwalimu / anafundisha wanafunzi
K
ii. Jina na Jina
Mfano: Baba na mama/wanakula
K
iii. Jina na kivumishi
Mfano: Mtoto mzuri/amepewa zawadi
K
iv. Kivumishi na jina
Mfano: Yule mwizi/amekamatwa
K
v. Kiswahili peke yake
Mfano: Wewe ni mzembe
K
vi. Kiwakilishi na kivumishi
Mfano: Yule mzembe / amefukuzwa
K
vii.Kitenzi jina na jina
Mfano: Kulia kwa mtoto/kunasikitisha
K
viii. Kitenzi jina na jina
Mfano: Kulia kwa mtoto/kunasikitisha
K
ix. Kitenzi jina na jina
Mfano: Kuungua kwa mtoto /kunasikitisha
K
x. Kitenzi jina na kivumishi
Mfano: Kuimba na kucheza kwake/kunafurahisha
K
xi. Jina na kishazi tegemezi kivumishi
Mfano: Mtoto aliyepotea /amepatikana leo asubuhi
K
xii.Nomino, kivumishi na kishazi tegemezi kivumishi
Mfano: Mtoto mzuri uliyemuona jana/ni ndugu yangu
K
xiii. Kivumishi nomino kivumishi na Bv
Mfano, Yule mtoto uliyemuona jana /ni mwanafunzi
K


KIARIFU (A)
Hii ni sehemu muhimu zaidi katika sentensi na wakati mwingine huweza kusimama peke yake bila kiima kwa kuwa hubeba viwakilishi vya kiima. Kiarifu ni sehemu katika sentensi ambayo hukaliwa na maneno ambayo huarifu tendo lililofanywa, linalofanywa au litakalofanywa na kiima.
Mfano: Mwalimu/anafundisha wanafunzi darasani
A
VIPASHIO VYA KIARIFU
i. Kitenzi kikuu peke yake
Mfano: Mtoto anacheza
A
ii. Kitenzi kisaidizi au visaidizi vilivyo sambamba na (T)kitenzi kikuu
Mfano: Mtoto alikuwa anataka kucheza
A
iii. Kitenzi kishirikishi na shamirisho
Mfano: Watoto/wanacheza uwanjani
A
Iv Kitenzi kikuu na chagizo
Mfano: Watoto/wanacheza uwanjani vizuri
A
v. Kitenzi kikuu shamirisho na chagizo
Mfano: Mwalimu/anafundisha wanafunzi darasani
A
vi. Kitenzi kisaidizi kikuu na shamirisho
Mfano: Mwalimu /alikuwa anafundisha wanafunzi wengi
A
vii. Kitenzi kisaidizi kikuu na chagizo
Mfano: Mwalimu/alikuwa nafundisha darasani
A
viii. Vitenzi visaidizi kikuu, shamirisho na chagizo
Mfano: Mzazi/alikuwa anataka kuwarudisha watoto wake nyumbani
A


∙ SHAMIRISHO (sh)
Shamirisho ni jina au kikundi jina (kirai nomino) kinachojaza nafasi ya mtendwa au mtenda, mtendwa katika sentensi. Shamirisho hutokea baada ya kitenzi kikuu au kitenzi kishirikishi katika sentensi,
Shamirisho hujibu swali mtenda amemtenda nani, Au mtendwa ametendewa nini?.lakini pia mtendwa ametendwa na nani?
Mfano: Wanafunzi/wanasoma vitabu
Sh
Juma/alimisomea Asha kitabu
Sh
∙ CHAGIZO (ch)
Chagizo ni sehemu ya sentensi ambayo hutokea upande wa kiarifu ambayo huwa na neno au kikundi cha maneno ambacho hujaza nafasi ya kielezi.
Mfano:Mama /amekwenda nyumbani
Ch


Mtoto /anacheza mpira vizuri sana
Ch

N:B Chagizo huwezakutokea mara baada ya kitenzi kikuu au mara baada ya shamirisho

Popular posts from this blog

FASIHI KWA UJUMLA NADHARIA YA FASIHI SANAA Sanaa ni uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifu umbo ambalo msanii hulitumia katika kufikishia ujumbe aliokusudia kwa jamii / hadhira. AINA ZA SANAA a) Sanaa za ghibu (muziki) Inategemea na matumizi ya ala za muziki (vifaa, sauti) uzuri wa umbo la sanaa ya muziki upo katika kusikia. Sanaa hii hailazimishi fanani (msanii) na hadhira kuwepo mahali pamoja kwa wakati mmoja. Mtunzi hufanya kazi kwa wakati wake na hadhira husikiliza kwa wakati wake. b) Sanaa za ufundi Sanaa hizi hutokana na kazi za mikono. (Mfano: uchoraji, ususi, ufinyanzi, uchongaji, uhunzi, utalizi/udalizi n.k.) Mfano; - uchoraji hutegemea sana kuwepo kwa kalamu, karatasi, kitambaa, brashi, rangi n.k. uchongaji huhitaji mundu, gogo, tupa, n.k. Uzuri wa umbo na sanaa za ufundi upo katika kuona. Sanaa hii hailazimishi fanani na hadhira kuwepo mahali pamoja kwa wakati mmoja. c) Sanaa za maonesho Ni kazi mbalimbali za Sanaa ambazo hutegemea utendaji (mfa...
MAENDELEO YA FASIHI SIMULIZI UWASILISHAJI NA UENEZAJI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI FASIHI SIMULIZI: Fasihi simulizi ni sanaa ambayo hutumia mazungumzo na matendo katika kuwasilisha ujumbe Fulani kwa watazamaji au wasikilizaji. Mazungumzo hayo huweza kuwa ya kuimbwa kutendwa au kuzungumzwa, Aina hii ya fasihi imepokelewa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo. Msimulizi katika fasihi simulizi mbali na kutumia mdomo wake hutumia viungo vyake vya mwili kama mikono, miguu, ishara mbalimbali katika uso wake na hata kupandisha na kushusha sauti yake. Kwa ujumla anaweza kutumia mwili wake mzima katika kuwasilisha na kufanikisha ujumbe wake kwa hadhira yake ambayo huwa ana kwa ana. Isotoshe anafaulu katika kutoa picha halisi ya dhana anayotaka kuiwasilisha kama ni ya huzuni, furaha, kuchekesha n.k. Zaidi ya kusimulia, kuimba na kuigiza msanii wa fasihi simulizi huwa na nafasi ya kushirikisha hadhira yake kama wahusika katika sanaa yake. Anaweza kutimiza hayo kwa kumfanya mshiri...
MAENDELEO YA KISWAHILI ASILI YA LUGHA YA KISWAHILI Neno asili lina maana kuwa jinsi kitu au jambo lilivyotokea au lilivyoanza na tunapozungumzia asili ya lugha ya Kiswahili ina maanisha tunachunguza namna lugha hiyo ilivyoanza. Wataalamu mbalimbali wa lugha wamefanya uchunguzi juu ya asili ya lugha ya Kiswahili. Uchunguzi huo umejenga nadharia mbalimbali zinazoelezea chimbuko la lugha ya Kiswahili. Kwa ujumla historia kuhusu asili ya lugha ya Kiswahili ina matatizo mengi na ndiyo maana kuna nadharia mbalimbali zinazoelezea juu ya asili ya lugha ya Kiswahili. Miongoni mwa matatizo yanayoikabili historia ya Kiswahili ni pamoja na: Hakuna uthibitisho kamili juu ya nadharia zinaelezea asili ya lugha ya Kiswahili na kuenea kwake. Uchunguzi wa asili ya Kiswahili ulifanywa na wataalamu wa kizungu ambao waliandika historia ya Kiswahili jinsi walivyoelewa wao baada ya kupata ushahidi kidogo tu. Wazawa hawakushirikishwa ipasavyo katika uchunguzi wa lugha ya Kiswahili. Hapakuwa na k...
VIAMBISHI Baadhi ya watu huchanganya dhana ya viambishi na dhana ya mofimu. Lakini ukweli ni kwamba mofimu na viambishi ni dhana mbili tofauti zenye mabwiano Fulani pia. Kwa ujumla viambishi vyote ni mofimu na mofimu zote ni viambishi SWALI: VIAMBISHI NI NINI? Viambishi ni mofimu zinazoandikwa kwenye mizizi wa neno ili kukamilisha muundo wa neno husika. Katika lugha ya Kiswahili viambishi vinaweza kuandikwa kabla ya mzizi wa neno na baada ya mzizi wa neno. kwa hiyo katika lugha ya kiswahili viambishi hutokea kabla ya mzizi wa neno na baada ya mzizi wa neno AINA ZA VIAMBISHI Lugha ya Kiswahili ina viambishi vya aina mbili VIAMBISHI AWALI/TANGULIZI Hivi ni viambishi ambavyo hutokea mwanzoni mwa mzizi wa neno na huwa ni vya aina mbalimbali A.Viambishi idadi /ngeli Viambishi hivi hupatikana mwanzoni mwa majina vivumishi kwa lengo la kuonesha idadi yaani wingi na umoja, Mfano : M – cheshi wa –zuri M – tu wa - tu Ki – ti vi-ti ...
AINA ZA SENTENSI Kuna aina kuu nne za sentensi Sentensi changamano Sentensi sahili/ huru. 3. Sentensi shurutia Sentensi Ambatano 1.SENTENSI SAHILI/HURU Hii ni aina ya sentensi ambayo hutawaliwa na kishazi huru. Kishazi hicho kinaweza kuwa kifungu tenzi kimoja ambacho kinaweza kuwa na kitenzi kikuu au kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu au kitenzi kishirikishi na shamirisho Mfano: Juma ni mzembe Juma alikuwa mzembe sana Mwalimu alikuwa nafundihsa darasani MIUNDO YA SENTENSI HURU /SAHILI Muundo wa kitenzi kikuu peke yake (tawaliwa) Mfano: Wanacheza Alinipiga Wanasoma i.Muundo wa kitenzi kikuu peke yake (tawaliwa) Mfano: Wanacheza Alinipiga Wanasoma ii.Muundo wa kitenzi na kitenzi kikuu Mfano: Alikuwa anasoma Walikuwa wanataka kufundishwa ii Muundo wa kirai na kirai kitenzi Mfano; Mwalimu anafundisha Wanafunzi wanamsikiliza iii. Muundo wa virai vite...
UTUMIZI WA LUGHA Matumizi ya lugha ni namna yakutumia lugha kulingana na mila, desturi na taratibu zilizopo katika jamii husika. Ni jinsi ambavyo mzungumzaji anatunza lugha kwa kuzingatia uhusiano wake na yule anayezungumza naye. Matumizi ya lugha hutegemea mambo kadhaa Kama vile: Uhusiano baina ya wazungumzaji. -Mada inayozungumzwa -Mazingira waliyomo wazungumzaji n.k Umuhimu wa matumizi ya lugha Kuwasaidia watumiaji wa lugha kutumia lugha kwa ufasaha Kumsadia mzungumzaji kuweza kutambua kutofautiana na kutumia mitindo mbalimbali ya lugha MTINDO WA LUGHA Mtindo wa lugha ni mabadiliko yanayojitokeza katika kutumia lugha mabadiliko ya lugha katika mitindo mbalimbali yaani mitindo mbalimbali ya lugha. Kwa kawaida mtindo wa lugha / mabadiliko katika kutumia lugha ndiyo inayomwongoza mzungumzaji katika kuelewa maneno na mitindo ya tungo, Matumizi katika lugha hutawaliwa na mambo ya...
MATUMIZI YA SARUFI NADHARIA ZA SARUFI Dhana ya sarufi ya lugha imefafanuliwa na wataalamu mbalimbali wa sarufi. Mtaalamu James Salehe Mdee (1999) sarufi ya Kiswahili sekondari na vyuo anafafanua maana ya sarufi kuwa ni mfumo wa kanuni za lugha zinazomwezesha mzungumzaji kutunga sentensi sahihi na zenye kukubaliwa na wazawa wa lugha. Kanuni hizi hujitokeza katika lugha ya mzawa wa lugha inayohusika ambaye anaifahamu barabara lugha yake. Sarufi inajumuisha mfumo wa sauti maumbo ya maneno muundo na maana. Mtaalamu Mbundo Msokile (1992) na khamisi (1978) wanasema sarufi ni mfumo wa taratibu na kanuni zinazotawala matumizi sahihi ya matamshi, maumbo ya maneno, miundo ya tungo na maanda ya miundo ya lugha. Ni mfumo wa taratibu zinazomwezesha mzungumzaji wa lugha kutoa tungo sahihi na pia inamwezesha mtu yeyote anayezungumza kuelewa tungo zinazotolewa na mtu mwingine anayetuma lugha hiyo hiyo. F. Nkwera (1978) anasema sarufi ni utaratibu wa kanuni zinazomwezesha mzawa au mtumiaji ...
KUBAINISHA MOFIMU Kubainisha mofimu ni kuligawa neno katika mofimu zinazolijenga neno na kueleza kazi za kila mofimu ubabaishaji huo wa mofimu hufuata hatua zifuatazo 1. Kutambua aina ya neno – Yaani kama neno hilo ni tegemezi au neno changamano, Neno huru huundwa na mofimu huru na neno tegemezi huundwa na mofimu tegemezi na neno changamano huundwa na moja huru na mengine tegemezi N: B Neno huru huwa halivunjwi vunjwi kwani huundwa na mofimu huru 2. Kulitenga neno na kulivunja vunja katika mofimu zinazojenga neno hilo yaani hujenga mofimu awali, mzizi na mofimu tamati. N: B Mofimu awali, mzizi na mofimu tamati hupatikana katika maneno tegemezi na maneno changamano 3. Kueleza kazi ya kila mofimu Mfano: Bainisha mofimu katika maneno yafuatayo Hatukupendi Hili ni neno tegemezi ii. 1- Mofimu awali kianzishi, nafsi ya kwanza wingi 2 - Mofimu awali rejeshi kwa mtendwa 3 - Mofimu awali rejeshi kwa mtenda 4 - Mofimu mzizi 5 ...
UTUNGAJI Maana ya utungaji Utungaji ni pato la akili ya mtu binafsi ambayo hurejeshwa kwa fani kama vile macho, ushairi, tamthiliya au hadithi. Utungaji ni kitendo cha kuyatoa mawazo ubongoni, kuyakusanya na kisha kuyadhihirisha kwa kuyaandika au kuyazungumza. Ni kitendo cha kuunda hoja na kuyapanga katika mtiririko unaofaa katika lugha kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii husika. SIFA ZA MTUNGAJI Mtunzi analazimika kuelewa kikamilifu mada inayoshughulikiwa. Mtungaji lazima azingatie kanuni na taratibu za uandishi. Mtungaji anatakiwa kuzingatia mpango mzuri na wenye mantiki wa mawazo kutoka mwanzoni hadi mwishoni. Mtungaji anapaswa kuwa na msamiati wa kutosha ili kumwezesha kutumia lugha bora, sanifu, na fasaha. Mtunzi anapaswa kuzingatia sarufi ya lugha anayoitumia. Mtunzi anapaswa kujali nyakati zinazofaa. Mtunzi anapaswa kuwa na uwezo wa kutosha wa kuhusisha yanayoelezwa na hali halisi ilivyo katika j...